Madhara ya riba yameelezewa kwa ufasaha kutoka vyanzo mbali mbali vya kidini na vile vya kijamii. Kama kawaida ya binadamu wameendelea kukaidi na kuipa riba majina tofauti ili ionekane nzuri lakini hilo halikufanikiwa kubadilisha uhalisia. 

Huwezi kufikiria hata mara mbili kwamba wakati umefika wa kutafuta mifumo mbadala ya kiuchumi ambayo itamkomboa binadamu na tatizo hilo. Ni leo tuu wabunge nchini Tanzania wamelalamikia kiwango kikubwa cha riba kama kikwazo cha kukopa benki.Tembelea gazeti la ‘Mwananchi’ Moja ktk malengo makubwa ya benki zinazo fuata maadili ya ki-Islam nikukataa riba ktk mazingira yake yote na badala yake hutumia mifumo ya kiuchumi mbadala ambapo mteja anagawana faida na hasara na benki. 

Uadilifu ktk jamii unapewa umuhimu mkubwa na mengineyo ambayo yanathamini uadilifu kwa pande zote zinazohusika. Kwa maelezo zaidi kuhusu benki, Saccos na uchumi unaofuata maadili ya ki-Islam tembelea http://ijuebankyakiislam.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2013

    WEWE ULIENDIKA HAPA LABDA HUJUI MAMBO YA BANKING AND FINANCE LAW, UNAFIKIRI KUTOKUWA NA RIBA NDIO KUTOKULIPA INTEREST KABISA KTK MKOPO, UNADANGANYIKA MY DEAR. ISLAMIC BANKING HAICHARGE RIBA LAKINI HAIMAANISHI HAULIPI ANY INTEREST ITS JUST IN ANOTHER NAME, BUT IN THE END YOU PAY THE LOAN PROBABLY EVEN HIGHER THAN YOU'D HAVE PAID NA HIYO RIBA. NAOMBA UFANYE UCHUNGUZI KABLA YA KUDANGANYIKA. MAELEZO ZAIDI ULIZIA WATAALAM MY DEAR THEY WILL LET YOU KNOW.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 11, 2013

    Soma maelezo vizuri bila kukurupuka, imeandikwa kwamba uchumi unaofuata maadili ya ki-Islam unatumia mfumo mbadala. Ni vyema ukafuatilia mifumo hiyo ikoje kwani malengo ya kukwepa riba sio kukwepa gharama ispokua ni kufanya kitu ambacho mfanyaji anajiridhisha kwamba ni sahihi. Kwa mfano unapoweka deposit ktk benki za kawaida kwa kiwango fulani na wakakuahidi kwamba watakulipa asilimia 8 riba kwa mfano, je wakipata hasara watakulipa nini na hapo ndio unaposikia benki imefilisika. Ni ngumu kukufahamisha ktk maelezo machache ispokua soma vizuri uchumi unaofuata maadili ya ki-Islam matatizo yako yataondoka.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 11, 2013

    Mimi nalaani riba kubwa zinazotozwa na mabenki yote hapa Tanzania. Nailaani pia BOT maana ndio mzizi wa riba hizo za ajabu na mfumuko wa bei. Sipati picha mwaka 2300 kutakuwa na noti za aina gani hapa nchini nikifikiria mwaka 1980 shilingi 20 ilikuwa noti yenye thamani kubwa!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 11, 2013

    Chapa ya mnyama hiyooooooooo taratiiiiiiiiiiiiiiiibu... Tunakaribia the coming of the ancient one, I AM himself.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 12, 2013

    Wee jamaa wa juu ha inaelekea lugha inapiga chenga. Pia huna habari za dunia watu wote siku hizi wanakimbilia kwenye islamic banking.wee bado una kasumba tafuta elimu na wewe ujue sio kupinga kitu

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 12, 2013

    Kwa hiyo na wewe sio mtalaam ila unazungumza kwa dhana na fitna, islamic banking isingekuwa better alternative insingekuwa moja ya masomo maarufu katika vyuo vikuu vya nchi za magharibi na pia isingefuatwa na kuekewa vikwazo vya kuifungua na bank zote za magharibi. Katika banking system na insurance system ambazo zina kuja juu kwa umaarufu mkubwa especially huku europe sababu zinaonekana kuwa reasonable and fair ni system za kiislam kwani wao ndio walioanzisha batter system na finance, if you don't know now you know usiwe unajaribu kuchallenge simply cos imetajwa islamic so and so boo. Mimi pia sio mtaalam wa finance na banking lakini ni academic, so I am aware.......ok!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...