Roboti inayokamua Ng'ombe maziwa Uholanzi. Mtambo huu unauzwa Euro laki moja na wakulima wa Uholanzi wanakopeshwa na Mabenki kwa riba ya asilimia tatu kwa mwaka na wanatakiwa kurejesha mkopo ndani ya miaka thelathini. Mtambo huu umeonyeshwa leo kwa Mabalozi wa Nchi za Afrika Uholanzi wanaotembelea maeneo mbalimbali ya Uholanzi.
Mabalozi wa Afrika Uholanzi Wakimsikiliza Mkurugenzi  Msaidizi wa Afrika wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi akiwaeleza jinsi Serikali ya Uholanzi inavyosaidia Wafugaji wa Ng'ombe wa Maziwa. Mwenye tai ya rangi ya taifa ni Balozi wa Tanzania Uholanzi, Ubelgiji, Luxemborg na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 14, 2013

    Haya sasa, mambo mazuri kama hayo badala ya kucopy na kuyaleta nchini kwenu mtaishia kushangaa tu na kurudi kama mlivyokwenda. Sijui nani ametuloga.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 14, 2013

    Balozi huna tai nyingineeee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...