Hivi ndivyo hali ilivyo ndani ya Ukumbi huu wa Nyumbani Lounge,Namanga jijini Dar es Salaam ambapo leo hii kuna bonge moja la show la Mwanadada mkongwe kwenye tasnia ya muziki hapa nchini,Lady Jay Dee ambaye anatimiza miaka 13 tangu alipoanza kazi yake ya muziki.katika show hii wanamuziki mbali mbali watapanda jukwaani aliwepo Mh. Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.
 Wadau mbali mbali wa muziki hapa nchini wapo ndani ya ukumbi huu hivi sasa kusuhudia show hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa muziki.
 Ndani ni nyomi la hatari,lakini nje nako watu bado wanataka kuingia huku wengi wao wakisema kuwa "hata kama hakuna siti,sie tuko radhi kusimama ilimradi tumsapoti Dada yetu.
 Getini mambo yako namna hii.
 Foleni bado ni ndefu na watu bado wanazidi kuingia ukumbini hapa hivi sasa.
Burudani ya Utangulizi ikiendelea.

Kwa picha na video zaidi zitawajia baadae kidogo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 15, 2013

    Sasa mbona kwa MwanaFAtuma hamuonyeshi bana?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 15, 2013

    Nasikiliza Mlimani patk- neema, Hiba, Nawashukuru wazazi wangu, Mv Mapenzi, etc: Marijana R. Ndoa ya mateao, Msondo-Solemba etc, YAP nipo ughaibuni, MLA MLA JANA MLA LEO KALA NINI???

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 15, 2013

    Sasa mbona kwa MwanaFAtuma hamuonyeshi bana?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 15, 2013

    Nimekubali!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 15, 2013

    Duh kumbe hii kitu ilikuwa kubwa namna...Nafikiri sasa naelewa kwa nini Clouds wanaleta wivu wa kike kutaka kubana watu wanaothubu kujaribu yale wanayofikiri wanayaweza wao tu. Go Babe Jaydee Go!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 15, 2013

    Jamani Clouds jifunzeni nini maana ya ushindani wa kibiashara.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 15, 2013

    Tuwe na tabia ya kuwa na vipaumbele katika maisha.Kukiwa na shughuli ya mchango wahisani kusaidia mwanafunzi akasome,au masikini asiyekuwa na uwezo baiskeli za walemavu wa viungo hutaona mtu hapo..Na baadhi ya watu hapo ndani wazazi wao vijijini hawana hata mlo mmoja kwa siku..na nyumba zao za matope zinakaribia kuanguka...Moyo kama huu wa "kutoa support" ni vema ukawa pia katika mambo muhimu zaidi ili kuweza kuundoa umasikini uliokithiri Tanzania..TAFAKARI..!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 15, 2013

    Ukiweka za Mwana Fa si ataona mmeamua kumtukana maana kulikuwa kweupe hamna watu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 15, 2013

    TUMESHA JIFUNZA:

    Huwezi kuiziba Riziki ya mtu!

    Dada wawatu naye amepata cha kwakwe licha ya kubanwa na Vigogo.

    Pamoja na malumbano yote na kubaniana lakini Ukumbi umetapika, ndio maana Nabii Suleiman aliomba kwa Mwenyezi apewe mamlaka ya kugawa Riziki lakini Mwenyezi kwa Busara akakataa kwa kuwa alijua jukumu likiwa mikononi mwa mtu itakuwa kaazi kweli kweli!

    ReplyDelete
  10. TEAM ANACONDA UKJune 15, 2013

    MUONYESHWE VITI MZIDI KUJITAVAIBU...WANAWAKE TUNAWZA BANA TUKITAKA

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 15, 2013

    Wanaotaka kumrudisha nyuma huyu msichana walaaniwe kwa nguvu zote. Nashauri TCRA iweke masharti magumu kwa vituo vya redio na television kuepuka hujuma na maslahi binafsi. Ukweli vituo vya redio na TV ni public hata kama umiliki ni binafsi.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 15, 2013

    Bifu za kutengenezwa na wasanii wa bongo zimeshamiri kama za wale wa USA. Zinasaidia Publicity though.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...