Na Abdulaziz Video,Nachingwea
Jumla ya Vijana 63 Waendesha Pikipiki na Bajaj (MAARUFU
BODABODA)Wilayani Nachingwea wamekabidhiwa Leseni za Udereva baada ya
kuhitimu Mafunzo yaliyotolewa na Veta na Kitengo cha Usalama
Barabarani baada ya Kuwezesha na Mbunge wa Jimbo hilo Ambae Pia ni
Waziri wa Sheria na Katiba,Mathias Chikawe.
Katika kufanikisha zoezi hilo Mbunge huyo pia amesaidia kuwalipia
Leseni zenye thamani ya Tshs Milioni Tatu ambapo Vijana 50 wamenufaika
na mpango huo ambao utakuwa endelevu katika jimbo hilo.
Mpango huo wa kuwezesha Vijana Hao ni Jitihada za Mkuu wa Wilaya Hiyo
Bi Regina Chonjo baada ya kukutana na makundi mbalimbali na kubaini
Baadhi ya Changamoto ikiwemo mahusiano mabaya kati ya Polisi wilayni
humo na Waendesha Bodaboda hali Iliyokuwa Inachangia Uvunjifu wa
AMANI Ikiwemo kutotoa huduma kwa Uaminifu Huku wakiwa ni tegemeo kubwa
la Usafiri na Usafirishaji Vijijini Wakiwemo WAGONJWA.
Mmoja ya Waendesha Boda boda akikabidhiwa leseni yake na Waziri wa Katiba NA Sheria,Mathias Chikawe katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Nachingwea.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Bi REGINA CHONJO akizungumza na Waendesha Boda boda wakati wa hafla ya kukabidhiwa leseni zao mara baada ya kumaliza mafunzo.Wa pili kulia ni Waziri wa Katiba NA Sheria,Mathias Chikawe.
Furaha baada ya kuhitimu mafunzo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...