Meza kuu wakati wa hafla hiyo |
Spika wa bunge Anne Makinda akizungumza katika hafla ya kumuaga Spika Mstaafu Samuel Sitta kwenye viwanja vya bunge Mjini Dodoma juni 21, 2013.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mheshimiwa Dr. Maua Daftari ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya hafla ya kumuaga Spika wa zamani,Mh. Samuel Sitta kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 21, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi zake pichani kwa Spika mstaafu. Samuel Sitta katika hafla ya kumuaga Spika huyo kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 21, 2013.Kushoto kwake ni mkewe Tunu na wengine kutoka kulia ni Mke wa Spika wa Zamani Margareth Sitta, Spika wa zamani Samuel Sitta na Spika wa Bunge Anne Makinda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Hii mpya. Miaka mingapi imepita?
ReplyDeleteAnaagwa kwani anaacha ubunge?
ReplyDeleteReally?? Now?? Its like wishing a happy b'day months later,,,c'on,,,They could make a better use of that money.
ReplyDeleteNext President Kwa hivyo lazima Waheshimiwa wampe heshima yake ndio kumuweka sawa. Amefanya mabadiliko kwenye bunge kwa kiasi kikubwa sana. Tumpeni pongezi zake. Mimi Mhe Sitta naona kwa mara ya kwanza Nchi yetu watu watapiga kura kwa kutofuata Itikadi zao kama Mhe Sitta atakuwa Mgombea wa Uraisi Kupitia Chama Cha Mapinduzi.
ReplyDeleteHuyo aliyekuambia ana gombea Urais ni nani? au una ota ndoto za kimweri? Mie sitaki kuona wazee wastaafu kujitekeza tokeza kwenye kugombea high positions. once umestaafu please take time to stay home and enjoy life with your family. halafu mie naona sasa hivi tuwaachie vijani hii nchi jamani, labda mabadiliko yatatokea haraka haraka, we so need a lot of changes in Tanzania. Tumechoka sana na mambo yale yale, sera zile zile, misemo ile ile......
ReplyDeleteNa makatibu wakuu wastaafu wa miaka yooote walikuwapo
ReplyDeleteNaungana na mtoa maoni wa kwanza hapo juu. Hicho kiti amekiacha baada ya miaka miwili na zaidi, kwa nini wanamuaga sasa hivi. Sipati mantiki hata kidogo. Ilipaswa aagwe walau katika mkutano wa kwanza wa bunge mara baada ya kumwachia kiti Mama Anna. Very poor planning of events
ReplyDeleteWewe ni makatibu wakuu wa wizara zote waliostaafu 4 years ago kuanzia hapo .Hapa mzazi karudi kutoka Dodoma na TV LED 66 inch na watapiga decoration nyumba nzima ( carpet na couches) na mzazi anafanya kazi consultant sehemu nyeti .
Delete