Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Linex akiwasalimia mashabiki na wapenzi wa Muziki waliofurika kwa wingi ndani ya Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma leo,ambapo usiku huu kulikuwa na bonge moja la Show ya Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013.
 Msanii aliejinyakulia Tuzo kadhaa za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013,Ommy Dimpoz akienda sambamba na timu yake ya Madansa wakitoa burudani ya kufa mtu ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma usiku huu.
 Msanii Ben Pol akighani moja ya nyimbo zake.
 Msanii wa Hip hop Mwenye tuzo nne za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013,Kala Jeremier akifanya vitu vyake usiku huu ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
 Mashabiki hawakutaka kabisa kupitwa na taswira za show hii.
 Ni shangwe kwa kwenda mbele ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma hivi sasa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2013

    Enzi zetu tukienda mziki tunacheza (selebuka), siyo siku hizi mnaenda halafy mnabaki kukudolea macho tu, mmeliwa hela yenu.Kama kusikiliza muziki si basi ikae nyumbani na nitausikiliza safi kabisa bila pigwa vumbi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...