Katika kuhakikisha riadha nchini Tanzania inafuta uteja kwa wakimbiaji wake kwa wafukuza upepo wa Kenya, Klabu ya Holili (HYAC) ya Mkoani Kilimanjaro imedhihirisha hilo katika Taveta Athletics Championship kwa kuwabwaga Wakenya katika mbio za meta 5000, 1500, 800 na 100.

Michuano hiyo ya Taveta imefanyika mwishoni mwa wiki katika Kaunti ya Taita-Taveta katika Mkoa wa Pwani nchini Kenya katika wilaya ya Taveta kwa kuwakutanisha wanariadha wa nchini Kenya huku Holili Youth Athletics Club ikialikwa kutoka nchini Tanzania.

Katika Mbio za meta 5,000 alikuwa ni Baraka Williams aliyekimbia kwa dakika 14:45:22 nafasi ya pili ikishikwa na Mtanzania mwingine Abubakar Joel aliyekimbia kwa muda wa 16:00:00 na nafasi ya tatu ikashikwa na Mkenya Kivoko Makao ambaye alikimbia kwa muda wa 16:34:00.

Wambura Lameck, Mtanzania kutoka katika klabu ya Riadha kwa vijana (HYAC) alionyesha uwezo katika mbio za meta 100 na 800 kwa wanaume; katika mbio za meta 100 Wambura alikimbia kwa muda wa sekunde 12:67 akiwatupa Wakenya Walter Kamujalo (13:12), Emmanuel Paulo (13:70) na Joseph Daudi (14:20).

Mbio za mita 800 Wambura Lameck alikimbikia kwa muda wa dakika 2:02:16 akimwacha Mkenya Ropya Nyingi ambaye alichukua muda wa dakika 2:04::14 na nafasi ya Tatu ikishikwa na Mtanzania kutoka HYAC Paulo Jackson aliyekimbia kwa muda wa dakika 2:05:98, Wakenya wengine Joseph Daudi (3:00:00) na Philip Matheka (3:04) walisshika nafasi mbili za mwisho.

Pia Watanzania waliwaonyesha kazi nyingine Wakenya katika mbio za meta 1500 pale Baraka Williams kutoka HYAC alipowakimbiza na kuongoza baada ya kumaliza kwa muda wa dakika 3:48:77 akifuatiwa na Mkenya Vicent Daniel kutoka Taveta aliyemaliza kwa kutumia muda wa dakika 4:16:85 nafasi ya tatu ikishikwa na Mtanzania mwingine kutoka HYAC Paulo Jackson ambaye alikimbia kwa dakika 5:04:66 na Mkenya Tumuna Ludovick akikimbia kwa muda wa dakika 5:09:07.

Kwa upande wa wanawake Watanzania Furaha Sambeke na Pendo Pamba walifanya kweli katika meta 800 kwa kushika nafasi mbili za juu.

Furaha Sambeke anayenolewa na Klabu ya Holili Youth Athletics alikimbia kwa muda wa dakika 2:30:00 na Pendo Pamba akimaliza kwa dakika 3:10, nafasi ya tatu ilishikwa na Mkenya Emily Wamboi na ya nne ikishikwa na Mkenya mwingine Cecily Kimale ambao wote walikimbia kwa kuda wa dakika 3:22:00 na 4:12:00.

Taveta Athletics Championship imefanyika ikiwa na makusudi ya kutengeneza Timu ya Riadha ya Taifa la Kenya ambako mchujo rasmi utafanyika Mjini Mombasa kwa watanzania walioshinda katika mbio hizo nao watakuwemo katika kinyang’anyiro hicho kwa ajili ya kupata uzoefu zaidi kutokana na ukweli kwamba taifa la Kenya limekuwa bora katika riadha barani Afrika. 

Mwandishi: JOHNSON JABIR, Moshi-Kilimanjaro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2013

    MUNGU IBARIKI TANZANIA. TARATIBU TUTAFIKA. TUNAHITAJI TU KUTILIA MKAZO MATAKWA YETU NA KUWA NA NIDHAMU KATIKA MATAYARISHO, PIA KUWAENZI WANARIADHA WETU.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2013

    Mbona muda wa mita 100 ni zaidi ya sekunde 12 mshindi kutoka Tanzania muda huo unatakiwa angalau uwe sekunde 10.0 ili kujiwekea matumaini.

    Pia kwa mita 800 muda wa dakika 2:02 ni muda wa pole sana maana wanariadha wa mita 1,500 hukimbia muda wa dakika 1:50 ambao kwa mita 1,500 ni muda ambao huwezi kupata medali ktk mashindano ya kimataifa.

    Inabidi vijana waelezwe kinaga ubaga kuwa wafanye mazoezi zaidi huku waki-focus kukimbia kwa muda unaokaribiana na viwango vya mashindano ya kimataifa au wachezaji wa kimataifa ili kuwa na matumaini ya kuipeperusha bendera ya Tanzania kw akupata medali na siyo kufukuza upepeo kama mbio hizi za Kauti ya Taveta huu nikufanya masihara.
    Mdau
    Wa-Viwango.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...