Dada Monica Luwondo (kulia) aliyewahi kufanya kazi katika gazeti la Daily News-Dar es salaam, sasa anaishi nchini Ghana, akihifadhi katika simu taarifa muhimu alipotembelea banda la Tanzania wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma Barani Afrika yanayofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Accra (AICC). Taarifa za kuwepo Watanzania hapo alisoma katika Globu ya Jamii
 Wakaazi wa Accra wakiwahi usafiri wa Umma maarufu kwa jina la Trot (Troti) kwa Dar ni Daladala, wengine wajasiriamali wakiingia mtaani kuwahi wateja katika vituo vya Daladala. Troti ni fedha iliyokua ikitumika awali kulipia usafiri huo, na manake ni kila mtu anaweza kulipa.
 Ni asubuhi na jamaa kapata tenda ya kurudisha mbwa katika kampuni ya ulinzi. Ukitaka huduma hiyo Accra unapiga simu inayoonekana ubavuni mwa gari, Mbwa lazima afungwe asidhuru wapiti njia au abiria katika magari mengine.
 Foleni sio Dar peke yake, hata Accra ipo!
 Moja ya matangazo makubwa katikati ya Accra likimanisha Ujauzito sio ugonjwa au hukumu ya kifo!
MAELEZO ya Ghana, nayo inashiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya Siku ya Utumishi Barani wa Umma Barani Afrika. Picha na mdau wa Globu ya Jamii, Florence Lawrence

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2013

    Inawezekana Ghana wameshaliona hili kuwa nchi za magahribi sasa wakina mama hwataki kubeba mimba wanahoji "Mtu hawezi kukaa kwenye mwili wangu miezi tisa, mimi sio punda!Hatari sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...