Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi
 SERIKALI imetoa wito kwa mamlaka ya mawasliano Tanzania TCRA kuangalia namna ya kupata mbinu mpya za kisasa katika kudhibiti wale wachache wanaojaribu kutumia teknolojia hiyo kuvunja umoja ,amani na utulivu. 
 Kauli hiyo ilitolewa jana na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama wakati wa semina ya siku moja iliyowashirikisha wakuu wa mikoa fanyika katika hotel ya Sarsalenero iliyopo mjini Moshi na kuwashirikisha wakuu wa mikoa pamoja na makatibu tawala wa mikoa ya Arusha,Tanga,Manyara na Kilimanjaro. 
 Gama alisema matummizi mabaya ya teknolojia ya mawasiliano sanjari na uwepo wa tovuti na Wavuti zinazo kiuka kuharibu mila,destuli na maadili ya mtanzania ni miongoni mwa changamoto zinazo ikabili sekta hiyo kwa sasa . 
 Alisema baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii na simu za mkononi katika kueneza fitna,chuki,matusi na uhasama miongoni mwa jamii ya watanzania jambo ambalo alisema TCRA inapaswa kuengalia eneo hilo kwa makini zaidi ili mitandao hiyo isije ikatumika katika kuwagawa watanzania. 
 Alisema ukuaji wa shughuli za kiuchumi zinazohusiana teknolojia ya mawasiliano ya habari zinaongezeka kwa kasi kubwa kanda ya kasikazini na kuwa kichocheo kikubwa katika sekta za Kilimo ,utalii na biashara katika mikoa ya kanda ya kaskazini sambamba na kupatikana kwa fursa mpya za ajira. 
 Awali akieleza malengo ya semina hiyo naibu mkurugenzi wa shughuli za kanda wa TCRA, Victor Nkya alisema mamlaka ya mawasiliano imelenga kujitangaza na kuwaelimisha wakuu wa mikoa juu ya shughuli za mamlaka hiyo ili kutambua haki na wajibu kama watumiaji wa mawasiliano.
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA ikiwahusisha wakuu wa mikoa na makatibu
tawala wa mikoa ya Manyara,Tanga,Arusha na Kilimanjaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...