Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akimpa zawadi ya sanamu ya twiga iliyotengenezwa  kwa vyuma chalavu, Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Hoang Quan, wakati wa chakula cha mchana kwenye mgahawa wa Akemi, jijini Dar es salaam. Sanamu hiyo ni ubunifu unaofanywa na kikundi cha walemavu jijini Dar es salaam (Picha zote na Bashir Nkoromo)
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha katika hoteli ya Protea Cortyard jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Hoang Quan, baada ya mgeni huyo na ujumbe wake kuwasili kwa ajili ya mazungumzo na Kinana, leo Juni 6, 2013.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  (wapili kulia) akizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam (CVP), Hoang Quan (wapili kulia), katika hoteli ya Protea Cortyard jijini Dar es Salaam. leo Juni 6, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Watatu kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Phili Mangula akizungumza wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya ujumbe wa Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Hoang Quan (wapili kushoto) katika Mgahawa wa Akemi jijini Dar es Salaam. leo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimshukuru Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Hoang Quan, baada ya mazungumzo yao katika hoteli ya Protea Courtyard, Dar es salaam, leo. Kushoto ni Dk. Asha Rose Migiro na watatu kushoto ni Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha katika hoteli ya Protea Cortyard jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Hoang Quan, baada ya mgeni huyo na ujumbe wake kuwasili kwa ajili ya mazungumzo na Kinana, leo Juni 6, 2013.
Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akimpokea Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Hoang Quan, kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo, Juni 6, 2013.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2013

    jamani hilo zawadi mlilompa si litapata kutu baada ya wiki moja tu?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2013

    jamani hilo zawadi mlilompa si litapata kutu baada ya wiki moja tu?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2013

    Jamani hawa Vietnam si ndio waliopigana vita na Marekani miaka ile? Sasa mbona CCM wanataka kutugombanisha na Obama?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...