Ujumbe wa wabunge watano kutoka Uingereza umewasili nchini na kutembelea Chuo Kikuu cha Dodoma kujionea mandeleo yake. Baada ya kupokelewa uwanja wa ndege wa Dodoma na Mwenyekiti wa CPA tawi la Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu, wabunge hao wakiwa na wenyeji wao walikutana na Makamu Mkuu wa UDOM Prof. Kikula na baadaye kufanya ziara fupi kwenye hospitali ya Chuo kitengo cha matibabu ya figo na sehemu ya utakasaji wa maji yanayotumika kwa upasuaji. Ziara ya UDOM iliitimishwa dhifa fupi iliyoandaliwa na Ofisi ya Bunge ikiongowa na Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ngugai pamoja na Katibu wa TWPG na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angela Kairuki katika Hoteli ya Dodoma.
Mwenyekiti wa CPA tawi la Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akiukaribisha Ujumbe wa wabunge watano kutoka Uingereza uliowasili nchini na kutembelea Chuo Kikuu cha Dodoma kujionea mandeleo yake.
Naibu Spika wa Bunge,Mh. Job Ndugai akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha wageni wao kutoka nchini Uingereza.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angella Kairuki akizungumza na ujumbe huo.
Lazima wafurahishwe maana sasa hakuna sababu kwanini WaTZ wende UK kusoma!!
ReplyDeleteOhhh Tanzania hatuna maendeleo!
ReplyDeleteOhhh Tanzania tupo nyuma!
Ohhh hii kuwa nyuma ni kwa sababu ya Chama Tawala, Ohhh hii kuwa nyuma ni kwa sababu ya Serikali iliyopo.
Mna hoja gani?
Acheni kuiweka nyuma Tanzania kwa kila kitu, HATUKATAI YAPO MAPUNGUFU KIDOGO, LAKINI acheni mchezo kabisa Chama Tawala na Serikali kazi wameifanya!
Wataalamu wa Elimu wametolea shavu UDOMM ndio haooo Waingereza !
Yaani wewe anonymous wa kwanza unataka kufananisha elimu inayotolewa na vyuo vikuu vya uingereza na elimu inayotolewa na UDOM kwa sababu wabunge wao wamefurahishwa sio wameridhishwa na UDOM. Mshkaji hatufikii hata 5% ya academic competence zao ndio maana kila mwenye nafasi anajaribu kwenda huko. Sisi mtu akipata elimu yake India anajiona hajambo na hao wahindi wamejaa huko wanalilia kupata elimu ya muingereza, tusitake kukimbia kabla hatujaweza hata kukaa tumejaribu kuongeza namba ya vyuo lakini kwa standard ya elimu Haa bado sana.
ReplyDeleteMaendeleoa ya division zero tele, au yapi? maendeleo ya mikopo ya kuingia University kwa tabu? Maendeleo ya barabara zilizobanana na foleni ya masaa kadhaa njiani? Maendeleo ya kupikia kuni na mikaa? Maendeleo ya kutokuwa na umeme wa uhakika? na kuwtokuwa na umeme vijijini? Maendeleo ya daktari mmoja kutibu wagonjwa 100 kwa siku? Maendeleo ya shule nzima kuwa na mwalimu mmoja tu? Au wawili? na mwalimu mmoja kufundisha wanafunzi 300? Maendeleo shule hazina walimu, zahanati hazina madaktari,
ReplyDeleteMiuondo mbinu tuliyonayo ni duni,Mishahara ya madaktari na waalimu ni midogo, wagonjwa mahospitalini wanalala chini, kina mama wanaojifungulia chini na sio vitandani? Maendeleo yapi hasa unayoyasema, mie naomba nisaidie kwani sielewi!