Naibu waziri Tamisemi,Kassim Majaliwa akifungua mkutano
wa vyama vya msingi na Ushika kikao ambacho kilitoa azimio la kujitoa
Ilulu Union na kuunzisha mchakato wa kuunda chama cha RUNALI UNION.
Baadhi wa wana Ushikia toka Amcos za
wilaya za Nachingwea,Liwale na Ruangwa wakiwa katika kikao cha pamoja
kuazimia kujitoa katika Ushirka wa ILULU.
Wajumbe 9 waliochaguliwa katika kikao hicho kuanzisha
RUNALI Union na kuwezesha chama hicho kusajiliwa ili kianze kazi Msimu
ujao wa mauzo ya korosho.
Na Abdulaziz Video-Nachingwea
Vyama 46 kati ya 51 vya msingi na ushirika vya wilaya za
Nachingwea,Ruangwa na Liwale,mkoani Lindi vimeazimia kujiondoa kwenye
chama kikuu cha ushirika cha mkoa wa Lindi cha Ilulu na kuanzisha
mchakato wa kuunda chama kipya cha ushirika cha wilaya hizo
kitakachojulikana kwa jina la RUNALI Union.
Uamuzi huo ambao uliozamiwa jana kwenye kikao kilichofanyika kwenye
ukumbi wa chuo cha ualimu Nachingwea chini ya uenyekiti wa Naibu
waziri ofisi ya waziri mkuu Tamisemi anayeshughulikia Elimu ambae pia
ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa,Kasimu Majaliwa ambapo viongozi vya
vyama vya msingi vya wilaya hizo waliridhia kwa kauli moja kuachana
na chama hicho cha ushirika cha Ilulu kwa kilichodaiwa kuwa
kimeshindwa kuwasaidia wakulima hata kusababisha wakulima wa korosho
washindwe kulipwa malipo yao yote ya pili kiasi cha kusababisha
uvunjifu wa amani na uharibifu wa mali za viongozi mbalimbali
wakiwemo viongozi wa vyama vya msingi na wa Chama cha Mapinduzi.
Akizungumza kwenye kikao hicho,Naibu waziri Tamisemi Kassim Majaliwa
alikitupia lawama chama kikuu cha Ilulu katika uendeshaji wake kiasi
cha kusababisha wananchi kuichukia serikali yao kwani viongozi wake si
waadilifu kwani wamekuwa wakijikusanyia kiasi kikubwa kupitia ushuru
mbalimbali zisizo za lazima ambapo alibainisha kuwa licha ya wakulima
kutopata malipo stahili chama cha Ilulu kimejipatia zaidi ya shilingi
Bilioni 9.9 huku wakulima wenye wakiangaika kupata malipo ya pili
Aidha kufuatia azimio hilo aliwaasa wanaushirika na Maafisa Ushirika
wa wilaya hizo kutorubuniwa kipindi cha mchakato wa Kuanzisha mchakato
wa Ushirika wa wilaya hizo zilizokusudia kujiondoa huku akiwataka
kuomba notisi ya kuitishwa kwa mkutano mkuu wa Ilulu ili vyama hivyo
vijiondoe kwa mujibu wa Sheria za Ushirika.
Makamu mwenyekiti chama cha msingi cha Umoja cha wilaya ya
Liwale,haguliwa kuwa makamu Mwenyekiti wa mchakato wa Kuanzisha RUNALI
alitaja baadhi ya mambo yaliyotajwa kuwa ni chanzo cha kujiondoa kwa
vyama hivyo vya wilaya tatu ni ukubwa wa eneo linalohudumiwa na Ilulu
jambo linalofanya chama hicho kishindwa kutoa huduma mzuri kwa
wanachama wake ucheleweshaji wa vitendea kazi yakiwemo magunia na
vitabu kwani Ilulu ndio waliojipa uzabuni pekee wa kusambaza huduma
hizo huku akieleza kuwa malengo ya Ushirika unaokusudiwa kuanzishwa
yatasaidia kupunguza baadhi ya Gharama zisizo lazima zinazokatwa Amcos
mbalimbali wakati wa mauzo ya Mazao.
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa,Bi Agness Hokororo alitoa wito kwa Wanasiasa
kuwafikia wakulima na kuwaeleza sababu za kuwepo kwa maendeleo ya
wakulima ili kuepukana na ujanja uliokuwa unafanywa na Ilulu kutokana
na Makato na upandishaji wa gharama mbalimbali za uendeshaji.
kikao hicho pia kilihudhuriwa na wabunge wa majimbo ya Liwale na
Ruangwa na wakuu wa wilaya hizo tatu ambao kwa nyakati tofauti
waliitaka kamati ya mpito iliyoundwa wajumbe 9 Chini ya Uratibu wa
Maafisa Ushirika wa wilaya hizo kuanzisha mchakato wa usajiri wa
RUNALI na kuharakisha zoezi hilo linakamilika haraka iwezekanavyo ili
chama hicho kipya kianze kazi ya ununuzi wa zao la korosho nje ya
Chama kikuu cha Mkoa ( ILULU) Msimu Ujao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...