Waziri Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Peter Mizengo Pinda, akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Sacoma group, Bwana. Sam Ochieng, namna ambavyo bidhaa za Matunda na Mboga mboga kutoka nchini Kenya zinavyopakiwa, kusafirishwa na hatimaye kuuzwa kwenye soko la Spitfield nchini Uingereza, kwa kupitia Jumuiya ya Sacoma. Umoja huo wa Sacoma wenye lengo la kuwakomboa wakulima wadogo wadogo wa africa ya Mashariki. Mheshimiwa Waziri Mkuu, alifanya ziara kwenye Soko la Spitafields, lililopo Stratford nchini Uingereza, kwa lengo la kujionea shughuli za Jumuiya ya Sacoma inavyoendesha shughuli zake kwenye soko hilo na jinsi ambavyo Jumuiya hiyo imeweza kuwasaidia Wakulima wa Matunda na Mboga kutoka nchini Kenya, kupata soko la kuuza Bidhaa zao hapa nchini Uingereza.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, akiangalia na kupata maelezo ya Ubora wa bidhaa unaotakiwa kupata soko nchini Uingereza. Pichani, mstari wa pili, (kwanza kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Ungereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe, kwanza (kulia) ni Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, Uingereza Bwana Yusuf Kashangwa, maofisa wa Ubalozi na Viongozi kutoka Tanzania ambao wameambatana na Waziri Mkuu nchini Uingereza kwenye Mkutano unaofanyika leo ambao unahusu jinsi ya kutokomeza njaa na umuhimu wa Lishe bora kwa Mama na Watoto Duniani (Hunger and Nutrition). Mkutano huo ambao umeandaliwa na Asasi za kiserikali na zisizo za Kiserikali, unakutanisha nchi kubwa Duniani, zijulikanazo kama G8, Wadhamini, Wachangiaji na Watoa misaada kwenye Asasi hizo, zenye lengo la kutokomeza njaa duniani na kusaidia kuwapatia Wamama na Watoto Lishe bora.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Soko la Spitalfields. Kushoto ni Meneja wa Masoko wa Kikundi cha Sacoma, Mama Perez Ochieng - Meneja wa Masoko wa Jumuiya ya Sacoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2013

    hayo ni maembe kutoka Tanga. Yanavushwa kupelekwa Kenya, wanapakia kwenye maboksi na kuuza Uingereza. Mheshimiwa Pinda tuletee contact za hao waingereza ili tuuze moja kwa moja toka Bongo. Wakenya wanapeta sana kwa jasho letu Watanzania lakini dawa yao iko jikoni.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2013

    Spitasfield haiko Stratford, iko Tower Hamletts off Commercial St karibu na Liverpool St, unless mmekwenda Market ya Hackney au nyingine.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2013

    Wee Anonymous wa pili, ndiyo umekosea. Spitalfields ziko nyingi, Uingereza. Mwandishi kaandika habari sahihi. Unayoongelea wewe siyo hiyo Waziri Mkuu aliyokwenda. Ya Liverpool str ambayo ndiyo inayofahamika zaidi haichukui mboga na matunda na kuyauza nchi nzima.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 10, 2013

    Ankal naomba contact za hao jamaa maana nina muhogo safi organic upo shamba tayari kwa kuvunwa, napatikana at mkulimabungu@gmail.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...