Na Anna Nkinda – Singapore
Watoto waliotengwa na jamii kutokana na tabia ya kutokuwa na maadili mazuri (watukutu) kama watapewa nafasi ya kupata mafunzo ya kutosha ya dini, elimu ya darasani na kuonyeshwa msingi mzuri wa maisha wanaweza kubadilika na kuwa watoto wema.
Hayo yamesemwa leo na Mama Sahnim Sokaimi ambaye ni mkuu wa kituo cha kurekebisha tabia za watoto wa kike watukutu cha PERTAPIS kilichoko nchini Singapore wakati akiongea na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipotembelea kituo hicho.
Alisema kuwa chuo hicho kinawapokea watoto wa kike kuanzia umri wa miaka 12 hadi 21 ambao mahakama imewakuta na makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na uvutaji wa sigara chini ya miaka 18, utumiaji wa madawa ya kulevya na kufanya biashara ya kuuza mwili (sexual activities).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...