Wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi na Taasisi zilizo chini ya Wizara wakiwa ndani ya Treni kuelekea katika kituo cha Buguruni Bahresa, ambapo waliadhimisha Wiki ya Mazingira Duniani kwa kufanya usafi katika eneo hilo leo asubuhi. Kauli Mbiu ya Wizara katika siku hii ni "Hifadhi maazingira kwa Uchukuzi Endelevu". Aidha Kauli mbiu ya Kitaifa ni 'Fikiri, kula; hifadhi Mazingira".
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Aman Kisamfu (wa pili kutoka kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi (wa tano kutoka kushoto) wakisubiria kuanza kazi ya Usafi katika eneo la Stehseni ya Buguruni Bahresa. Wizara ya Uchukuzi na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wamefanya usafi kwenye eneo hilo leo asubuhi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani mbayo kitaifa inaadhimishwa Mkoani Rukwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira na Usalama wa Usafiri Majini, Bi. Tumpe Mwaijande (aliyeshika mfuko) akifanya usafi katika eneo la Buguruni Bahresa kama ishara ya kuadhimisha Wiki ya Mazingira Duniani. Wafanyakazi wa wizara ya Uchukuzi pamoja na taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walifanya usafi katika eneo hilo kama ishara ya kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani ambapo Kauli mbiu ya Wizara hiyo ikiwa ni "Hifadhi Maazingira kwa Uchukuzi Endelevu".
Wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi na taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakifanya usafi katika Stesheni ya Buguruni Bahresa kama ishara ya kuadhimisha wiki ya Mazingira Duniani, Zoezi hilo la kufanya usafi limebeba kauli mbiu inayosema "Hifadhi Maazingira kwa Uchukuzi Endelevu".
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira na Usalama, Bi. Tumpe Mwaijande akiongea na wafanyakazi wa Wizara na taasisi zilizo chini ya Wizara (hawapo pichani) hiyo baada ya kumaliza zoezi la usafi katika eneo la Buguruni Bahresa leo asubuhi. Pamoja na zoezi la Usafi Wizara ya Uchukuzi ilikabidhi Majembe, mafyekeo na reki kwa Shule ya Msingi Hekima na Zahanati ya Buguruni.
Hhahahaha hahahha wenye majukumu yao wamelala?au wanahubiri siasa?kungekua kusafi nadhani...........
ReplyDelete
ReplyDeleteBAHRESA aibu! na FIKIRI KABLA YA KUTUUZIA CHAKULA! eneo linalozunguka kiwanda chako cha chakula kichafu kiasi hicho mnajali pesa tu wenye viwanda wangebanwa kuhusu maeneo yanayowazunguka Bahresa unasubiri sikukuu ya Idd ukatoe mbuzi na unga wa ngano tu?? JALI MAZINGIRA FIKIRI KABLA YA KULA. wafanya biashara pale aibu! mabwana afya aibu!mnapokea mishahara bure hamna lolote hata kutoa elimu kwa wafanya biashara wasafishe mazingira? na wakisafisha watupe wapi taka? AIBU! AIBU! AIBU!
Au mnasubiri Wazungu waje watoe mkopo msafishe mazingira?
HA! HA! HAAAAAAAAaaaaaaaa! yaani vijana wa sasi hawajui tofauti ya TAZARA na RELI YA KATI! TAZARA haipiti buguruni bakhresa!
ReplyDeleteWote hao wanauza sura tu. Kwanza wengine ukienda majumbani kwao kunanuka uozo wanakaa kusafisha kwingine. Shame on you.
ReplyDelete