ASKARI WA JESHI LA ULINZI WAKISAIDIA KUONDOA MAJERUHI  KATIKA ENEO LA AJALI ILIYOTOKEA LEO ENEO LA MWANAKWEREKWE BAADA YA GARI MOJA  MSAFARA WA MAZISHI KUPINDUKA KARIBU NA SOKO KUU LA MWANAKWEREKWE UMBALI WA MITA MIA 300 KUTOKA MAKABURI YA MWANAKWEREKWE WALIKOZIKWA WANAJESHI WALIOUAWA DARFUR.
 MAJERUHI ZAIDI WAKIONDOLEWA ENEO LA AJALI KUPELEKWA HOSPITALI

GARI LILILOPATA AJALI. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. INNA LILLAH WAINNA ILAYHI RAJIUN. Poleni sana, maana ni msiba juu ya msiba. Hata hivyo liandikwalo na MOLA abadan kulikwepa. Mwenyeez Mungu awaghufirie kwa yote na awapumzishe pema peponi - AMEEN. Na majeruhi wote awajaaliye takhfifu INSHA ALLAH, waweze kupona haraka.

    Ila kwa maoni yangu, ningeomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hebu ijaribu kuimarisha usalama wa barabarani khasa katika eneo hilo la hapo Kwerekwe (Mwanakwerekwe) sokoni, maana pamezidi msongamano wa vyombo vya barabarani, utakuta magari ya shamba, madaladala, marikwama, mabaskeli bado hao wendao kwa miguu na hizo Vespa zilizojazana, hata ukiangalia ufinyu na udogo eneo hilo na hata wa barabara pia vinachangia zahma kama hizo kutokea. Poleni wote mliopata ajali na Pole kwa wafiwa na watanzania wote kwa jumla.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2013

    Inna lillah wa inna ilayhi rajiun, Muumba awape subra wafiwa na waliopata na ajalia. Ajalie wapone haraka na waliyefariki awajaaliye wawe miongoni mwa waja wema

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2013

    Poleni kwa sote. Haya magari ya jeshi na vyombo vya ulinzi na usalama yangekuwa yanasimamiwa kikamilifu kuhakikisha yanakuwa salama yawapo barabarani.

    Usikute magari haya ni mabovu, yamekosa ubora, break,taa, na kadhalika na yakawa yanatembea barabarani tena kwa ubabe na mwendo wa kasi sana kisa ni gari la dola wakati dola yenyewe ni ya wananchi ambao ndio wenye mamlaka kisheria.

    lazima tubadilike ujumbe kwenu wahusika.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2013

    Inna lillah wa inna ilayhi rajiun, Muumba awape subra wafiwa na waliopata na ajalia.
    Ajalie wapone haraka!

    Ila na JWTZ iache dhuluma kwa watu na maisha ya watu maana "kwa Mungu si kwa Mzungu" waweza dhulumu maisha ya Mtu mtu mnonge Mtwara ukaiona joto yake au malipo yake Darfur au popote pale ikiwa kama haukufata haki!

    Wajaribu kutendea binadamu wenzao HAKI katika utekelezaji wa majukumu yao!

    Maana hapa duniani hakuna aliye juu ya mwingine kwa upande wa Mungu!

    Hivi mali, vyeo, madaraka, fedha nk ni mapambo tu ya hapa hapa duniani na kama utayatumia vibaya ni hatari sana!

    Yaweza kusababisha mishangao mingi tu! Kwa mfano, Kwa nini tulioenda kuwalinda watushambulie, kwenda/kutoka mazishini magari yanapinduka na etc.

    Tutendeni haki ktk majukumu yetu, na hii si kwa JWTZ tu ni hata kwa POLISI, WANASHERIA, MAHAKIMU, WAAJIRI, WAPELELEZI WA KESI, na kadhalika!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 24, 2013

    Hapa umegusa waajiri nimefurahi sana. Maana siku hizi ajira hupati mpaka umkubali mwajiri.
    Kama umeajiriwa ili uongezwe mshahara lazima aidha ukubali matakwa ya bosi wako: kama ni kuiba mali ya kampuni ukubali kushirikiana naye.

    Hii inachangia pia amani kitoweka pale inapogunduliwa na wahanga.

    Poleni sana wafiwa. tuwataadhali watoto wetu wawe na mwenendo mwema ktk jamii ili majanga wayaepuke

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 24, 2013

    Hapa umegusa waajiri nimefurahi sana. Maana siku hizi ajira hupati mpaka umkubali mwajiri.
    Kama umeajiriwa ili uongezwe mshahara lazima aidha ukubali matakwa ya bosi wako: kama ni kuiba mali ya kampuni ukubali kushirikiana naye.

    Hii inachangia pia amani kitoweka pale inapogunduliwa na wahanga.

    Poleni sana wafiwa. tuwataadhali watoto wetu wawe na mwenendo mwema ktk jamii ili majanga wayaepuke

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 24, 2013

    POLENI WAFIWA . MOLA AWAREHEMU WOTE WALIOPOTEZA MAISHA.

    HATUWEZI KUJUA MIPANGO YA MUNGU.YEYE HUWA NA MIPANGO YAKE.

    lakini hawa wanajeshi na mapolisi wananyanyasa wananchi. Wanadhulumu mali na kubaka. Siwahukumu , ila hivi ni vitendo ambavyo kila mtu huviona na vinakatazwa ktk jamii.

    Lakini wenzetu wanajeshi na polisi hujiona kuwa wako juu ya sheria.Hata wakikamatwa na kufikishwa polisi, wvombo vya dola huwalinda. Sasa sisi raia tumebaki kulindwa na Mungu

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 24, 2013

    Kwa Mungu si kwa mzungu - lol usemi umenikuna sana huu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...