Habari ya kazi ndugu zangu.

Ninayo furaha kuwajulisha ya kwamba sasa kazi zangu zote za muziki zitakuwa zinapatikana kwenye mitandao yote ya kununua nyimbo za wasanii duniani. Tayari nishasambaza Album yangu ya kwanza " Pwaa The Album" na singles zingine kama "Hmmm", na "Mambo" kwenye mitandao ifuatayo:

 iTunes, Amazon MP3, Spotify, Google Play, Xbox Music, Deezer, Rhapsody, Simfy, MySpace Music, Nokia, Wimp, Sony Music Unlimited,Napster, Verve Life, Media net, Shazam,eMusic, iHeartRadio, Muve Music, and Rdio.


kwa wale mliokosa nafasi ya kujipatia nakala za album yangu ya kwanza, hii ni fursa kwenu kujipatia Album hiyo kupitia mitandao hii kwa bei nafuu sana. Tupeane support ili tukuze muziki wetu.

kwa sasa namalizia kurekodi album yangu ya pili ambayo ipo kwenye mahadhi ya kimataifa zaidi na punde ikikamilika  ntaanza kuachia single moja moja kupitia mitandao hii, mitandao ya simu kwa njia ya RBT na  pamoja na wa "The Kleek" chini ya mkataba wangu mpya na Universal Music Group.

Asanteni sana na hii hapa ni link ya 
kupata nyimbo zangu zote kupitia iTunes.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2013

    huyu jamaa naona anatumia muda mwingi zaidi kuji commercialize kuliko kukaa studio na kutoa track nzuri! hivi ni mwimbo gani hasa wa huyu jamaa ambao ni hit!?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...