Ijumaa hii Ankal alitembelea Chuo cha Maafisa wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (Tanzania Military Academy - TMA) huko Monduli, Arusha, na kukutana na baadhi ya wadau wakubwa wa Globu ya Jamii ambao wapo chuoni hapo wakibukua. Ankal alifarijika sana kukuta kuwa hata maafande sio tu ni wafuatiliaji wakubwa wa Libeneke hili bali pia walimshauri aendelee kuheshimu maadili pamoja na sheria na kanuni za taaluma ya habari, ikiwa ni pamoja na kuendelea kuepuka kujeruhi hisia za mtu ama watu, jambo ambalo wametaja kuwa ni moja ya siri za mafanikio haya kiasi yaliyopatikana.
Ankal akiwakumbusha wadau hao wa TMA kuwa Septemba 8, mwaka huu Globu ya Jamii itasherehekea miaka tisa toka izaliwe kule Helsinki, Finland, na akawakaribishwa kwenye sherehe za kukata na shoka ambazo zinaandaliwa. Stay tuned...Libeneke Oye!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2013

    Oyeeeee Libeneke!

    Ankali huo ubwabwa na Libeneke itatakiwa wana libeneke wa ukweli ndio waulena waalikwe sio kiuwaaloka wauza sura.

    Ankali tumia utaratibu huu kuwapata wana libeneke wa kweli ambao hutembelea Jamvi hili.

    Ongea na wataalamu wa ICT wataweza kukupa vigezo vya kumjua mfuatiliaji wa Libeneke MOJAWAPO NI KUPITIA KOMPUTA ANYOTUMIA ITAWEKA REKODI YA MARA NGAPAI ANAINGIA JAMVINI.

    HIYO KITU INAWEZEKANA HATA KWA WAZEE WA INFORMATION INTELLIGENCE WANAWEZA KUJUA LAKINI KAMA SUALA LA KISHERIA LIKIHITAJIKA LINAWEZA KUSHIRIKISHWA MAMLAKA YA MAWASILIANO NCHINI TCRA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2013

    Ankal umeenda kufanya nini huko monduli na wewe siyo askari?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 15, 2013

    Mdau wa Kwanza Ankali anaweza kuwaambia TCRA waangalie IP addresses za Blogu na kutoa ''Terrestial Data'' hasa ktk upande wa Maoni ili kujua ni nani ametoa Maoni zaidi na Kigezo nikuwa MWANA LIBENEKE NI YULE AINGIAE JAMVINI SIO KUSOMA PEKE YAKE BALI NA KUTOA MAONI, HIVYO POSTINGS ZIKIFANYIKA TCRA KTK SYSTEMS ZAO ZINAWEKA RECORDS.

    Lakini tusije kiangukia upande wa EDWARD SNOWDEN aneyesakwa na Obama kwa kuvujisha siri za nchi Marekani, sisi tutafanya kwa ridhaa za Wana Libeneke wenyewe.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 15, 2013

    Mjomba Michuzi ama kweli upo Serikalini hadi umewafikia Wapiganaji huko?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 15, 2013

    Mdau wa 2 unaionaje Suti aliyovaa Ankali?

    Si ndio mulemule mipango ya Kiserikali?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...