Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  imesema mpango wa utekelezaji uanzishaji wa Anwani za Makazi na Misimbo ya posta itasaidia kurahisisha mawaslimo na kuchochea maendeleo nchini.
Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo, Profesa Patrick Makungu aliwambia wanandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam mara baada  ya kufungua semina ya siku moja ya wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa wizara, juu ya kuwajengea uelewa pamoja na kuhamasisha matumizi ya anwani za makazi na misimbo ya posta..
“Jambo hili ni muhimu sana katika ulimwengu wa sasa katika kurahishsisha mawasiliano na maendeleo,” na aliongeza kusema kwa jiji la Dar es Salaam ni mhimu zaidi sababu huchangia asilimia 70 ya mapato ya kodi.
Alisema awamu ya kwanza ya mpango huo kwa jiji la Dar es Salaam ilizinduliwa rasmi na Septemba 14, 2012 na Rais Jakaya Kikwete ambapo utekelezaji wake unahusisha serikali taasisi za serikali, taasisi zisizo za kiserikali na sekta binafsi.
Alisema mkoa wa Dar es Salaam umeanza kutekeleza mpango huu ambapo tayari baadhi ya wizara na taasisi zimezana kutumia misimbo hiyo ya posta na wananchi wahamasike kuupokea .
Alisema kamati tendaji kwa kushirikiana na wizara ya mawasiliano ,sayansi na tekonolojia na mamalaka ya mawasiliano Tanzania, Shirika la Posta, Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam na wadau mbalimbali wameandaa mipango ya utekelezaji katika jiji nzima.
Mkurugenzi Maswala ya Posta Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Bi.Rehema Makubwi alisema program hiyo itasaidia huduma za posta kuimarika ambapo mwananchi atapata barua na vifurushi kwa urahisi zaidi.
”Pia inasaidia katika kutambua wananchi walipo, na wakati wa dharura ya majanga kama magonjwa na moto kupata huduma kwa urahisi ,” na hii ndiyo mfumo nzuri zaidi katika kukabili maswala haya.
Aliongeza kusema pia itawawezesha wafanyabiashara kupata mikopo benki kwa urahisi kutokana anwani ya makazi na misimbo ya posta huruhisisha mawasiliano ya kuwapata.
Naye, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Uchukuzi, Bw.Issa Nchasi alisema mpango huo katika wizara yake umefika wakati mwafaka kwani ita rahisisha na ni mwongozo wa kitaifa wa uwekezaji wa majina ya mitaa na namba za nyumba.
“ Hii itaongeza ufanisi katika Mamlaka ya usimamimizi wa  Bandari na Maziwa (TPA) mizigo au bidha kumfikia mmiliki moja kwamoja,” bila ya kubahatisha alipo kutokana na kuwepo kwa anwani za uhakiaka.
Mpango huo ulitekelezwa kwa majaribio katika kata nane za Manispaa ya Arusha  na Manispaa ya Dodoma kata saba na sasa unateklezwa jijini Dar es Salaam kwa kuanzia na majengo ya Serikali yote ili kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2013

    Kwa kweli ni jambo zuri sana ambalo litasadia hata ufanisi kwenye ulipaji kodi na mabo mengine ya traccking. Ila walisha fanya ushindanishi ( Tender) kwa kampuni zitakazo fanya kazi hii kupitia TCRA. Na wakasema mradi wa kujaribu utaanza tarehe moja julai 2013 kwa Manisipaa ya Kinondni. Mpaka leo TCRA hawajotoa mshindi wa tenda hiyo. JE NDO KAWAIDA YA KI-BONGO BONGO??? Mfuba bila nyama. I mean maneno bila utendaji??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...