Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula akiwa na Rais Barack Obama mara baada ya kuwasilisha hati ya utambulisho katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama White House jijini Washington DC 
IMG_3118
Mama Balozi Liberata Mula mula akipokelewa na mama Munanka baada ya kukutana na kujitambulisha kwa rais Obama huko White house alhamisi. Balozi Mula mula alitoa shukrani za dhati kwa mabalozi wenzake waliofika kumpongeza pamoja na Mh.EL mbunge wa Monduli na watanzania wote waliokuwapo kwa kuhudhuria hafla hiyo. Pamoja na mambo mengine alieleza pia kushangazwa kwake na kufurahishwa na mapokezi yasiyo na makuu yalio ya kifamilia zaidi aliyopewa huko White house na Rais Barack Obama na familia yake alipowasilisha hati zake za utambulisho siku ya alhamisi Julai 18. IMG_3168
Mama Balozi Mula mula akiwa na mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa bunge la Tanzania na mbunge wa Monduli Edward Lowassa. IMG_3143
Mchungaji Shideko akifungua kwa sala. IMG_3125
Mc wa shughuli hiyo Mindi Kasiga na afisa habari ubalozini akitoa utaratibu. IMG_3164
Mama Munanka akiwa na Raymond Maro. IMG_3153
Mama Mulamula akiitambulisha familia yake. IMG_3145 
Balozi wa Rwanda nchini Marekani Prof.Mathilde Mukantabana akisikiliza kwa makini. IMG_3178
Shamis akiwa na balozi wa Burundi nchini Marekani.Kwa taarifa zaidi bofya www.sundayshomari.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hongera sana Balozi Mulamula tunakutakia mafanikio mema katika majukumu uliyokabidhiwa na Mhe. Rais, tunajua kwamba wewe ni mchapakazi na utafanikisha vizuri. Yes you can Madame Ambassador. God bless you and your family. The Kiondos.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 19, 2013

    wapiga picha jaribuni kuwarekebisha viongozi wetu kabla yakuwapiga picha. mfano suti ya muheshimiwa inaonekana vifungo vya kati vikiwa wazi.au ndio miondoko ya marekani?.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 19, 2013

    mtoa maoni wa pili. Kawaida koti la suti huwa halifungwi vifungo vyote. Sio Marekani tuu ni kwa mvaaji yeyote makini wa suti hivyo mheshimiwa Lowasa yuko poa, amepatia.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 19, 2013

    "Anonymous said...'
    wapiga picha jaribuni kuwarekebisha viongozi wetu kabla yakuwapiga picha. mfano suti ya muheshimiwa inaonekana vifungo vya kati vikiwa wazi.au ndio miondoko ya marekani?'"


    July 19, 2013


    Achana na tabia ya kuwa too much fashionista; hufai!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 19, 2013

    Kweli, Rais Obama ameipa Tanzania nafasi ya kuwa kwenye jiko la mbele...ikiwa ni pamoja na "fasta, gasta" ya ku-present accredition.
    Maana ma-balozi wengine huweza kuchukua miaka kabla ya kupata hiyo nafasi kutokana na shughuli nyingi za Rais wa Amerika!

    ReplyDelete
  6. BihalamuloJuly 20, 2013

    Huo yiko na Shamis sio balozi wa Burundi. Rekebicheni captions zenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...