Bw. Mustafa Haji Abdinur mwandishi kutoka Somalia anayeandikia AFP akizungumza mbele ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, wakati Baraza hilo siku ya jumatano lilipojadili usalama wa waandishi wa habari katika maeneo yenye migogoro, Bw. Abdinur ambaye amejifundisha mwenyewe uandishi wa habari alieleza kwamba pale alipo ni kama maiti inayotembea na kwamba ni suala la muda tu yeye kuuawa kutokana na ukweli kwamba waandishi wenzake wengi wamekwisha kuuawa nchini Somalia. Hii ili kuwa ni mara ya kwanza kwa waandishi wa kimataifa kuzungumza ndani ya Baraza hilo
Bw. Richard Engel kutoka NBC News mmoja kati ya waandishi wanne walioalikwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kueelezea uzoefu wao na mikimikiki wanayokumbana nayo wanapotekeza majukumu yao ya kiuandishi. Bw. Engel ambaye amesema amewahi kutekwa, alilitaka Baraza Kuu la Usalama linapojadilia kuhusu dhana nzima ya usalama wa waandishi, kujadili pia ni nani hasa mwandishi wa habari anaye stahili ulinzi na akahoji kama wanaharakati ambao nao wanachukua picha za matukio mbalimbali na kuzipost kwenye mablog kama nao ni waandishi wa habari. pembeni yake ni Bi. Kathleen Carroll, ambaye ni mhariri mtendaji wa Associated Press na Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Kamati ya Kulinda Waandishi ( CPJ) yeye katika mchango wake alisema licha ya kwamba waandishi wengi wanapoteza maisha wakati wakitafuta habari kwenye maeneo yenye migogoro lakini waandishi watano kati ya sita wanauawa ndani ya nchi zao wakati wakitimiza majukumu yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...