Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa mtabiri bingwa wa kwanza wa hali ya
hewa na mkurugenzi mkuu wa kwanza wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Bw. Urban
Blass Lifigahani (Pichani). Hayati Lifiga alizaliwa
tarehe 27 Novemba 1936, kifo chake kilichotokea Jumatatu tarehe 15 Julai 2013
mchana katika hospitali ya Bosph Mbezi kwa Msuguli Dar es Salaam.
Bwana Lifiga alikuwa mtabiri bingwa wa
kwanza Tanzania na Mwaafrika wa kwanza kujiunga Idara ya Hali ya Hewa ya Afrika
Mashariki iliyokuwa chini ya Jumuia ya Afrika Mashariki, ambayo kwa wakati huu
makao yake makuu yalikuwa Nairobi, Kenya. Bwana Lifaga aliteuli kuwa Mkurugenzi
Mkuu wa kwanza wa iliyokuwa Idara Kuu ya Hali ya Hewa, Tanzania. Alishisiriki
na kushauri Serikali katika kuanzisha kwa Idara hiyo.
Pamoja na nafasi ya Mkurugenzi Mkuu pia
alichaguliwa kuwa Mjumbe wa kudumu wa Tanzania katika Kamati Kuu ya Shirika la
Hali ya Hewa Dunia. Nafasi nyingine aliyeishika wakati wa uhai wake ni Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Hali ya Hewa ya Afrika Mashiriki.
Bwana Lifiga atakubumbuka kwa mchango wake
mkubwa katika kuendeleza sayansi ya hali ya hewa nchini, Afrika na Duniani.
Ni mmoja kati ya wanasayansi waliokuwa zao
la chuo kikuu cha Makerere na alichukua shahada ya udhamili chuo kikuu cha
Nairobi. Hapa nchini alipata mafuzo ya Sekondari katika shule za Kwiro
Sekondari, Mahenge na Pugu Sekondari, Dar es salaam.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika Ijumaa
tarehe 19 Julai 2013 nyumbani kwake Msakuzi.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inajumuika
na familia, ndugu, jamaa na marafiki katika kuomboleza msiba huu.
Bwana ametoa, bwana ametwaa, Jina lake
lihimidiwe; AMENI
IMETOLEWA
NA OFISI YA UHISIANO MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...