Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto), akiwa na Makamu Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk Mussa Assad (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji NBC, Mizinga Melu katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake mjini Zanzibar jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr Ali Mohamed Shein (kulia), akichukua futari katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mjini Zanzibar jana.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bi. Mizinga Melu katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa wateja wake mjini Zanzibar jana. Kushoto ni Meneja Mkuu Kitengo cha Uhusiano cha benki hiyo, William Kallaghe.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar, Zahra Ali Hamadi (kulia), Katibu Mkuu katika wizara hiyo, Mwanaidi Saleh Abdallah (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kushoto) wakichukua mlo wa futari iliyondaliwa na benki hiyo mjini Zanzibar jana.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kulia) akilakiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk Mussa Assad katika hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC Kwa wateja wake mjini Zanzibar jana. Katikati ni Meneja Mkuu Kitengo cha Uhusiano cha benki hiyo, William Kallaghe.
Mjumbe wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk Kassim Hussein (kulia) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdallah Mwinyi Khamis baada ya hafla ya futari waliyoiandaa kwa wateja wao mjini Zanzibar jana. Nyuma ya Dk Kassim ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Mizinga Melu.
Baadhi ya waalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Kisiwani Zanzibar jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...