kocha kwame mkuluma kulia akimwelekeza Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' jinsi ya kutupa makonde mazito mazito.

Na SUPER D

 Bondia  Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' yupo kambini kwa ajili ya kupambana na bondia Bahati Mwafyela mpambano utakaofanyika siku ya sikukuu ya Iddi pili jijini Dar es salaam,katika ukumbi wa friends Corner Manzese.

 akizungumzia maandalizi ya mpambano huo mtaalishaji wa Mpambano huo,Waziri Rosta amesema mpambano huo wa uzito wa juu umekuwa gumzo katika jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake kwani mabondia hao wanatafutana kwa muda mrefu sana na sasa wamekutana kwa ajili ya mchezo huo.

Mpambano huo wa raundi 8 siwakukosa kwani ndio mpambano pekee kwa mwaka huu kukutanisha uzito wa juu kwani mabondia wa uzito huu  wanaotamba viwango vyao ni vidogo ukizingatia kuwa wapo wachache nchini.

aliongeza kuwa mbali na mpambano huo kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia chipkizi na wanaotamba hapa nchini.

Na kwa upande wa kocha anaemnoa bondia  Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' amesema kuwa bondia wake alikuwa na manyama nyama mengi lakini kwa sasa hakuna kutokana na mazoezi anayompatia kwani kwa sasa dozi yake ni kutwa mara tatu na mpaka siku ya mchezo nahisi mambo yatakuwa safi.

Mpambano huo utakao sindikizwa na mabondia Hassani Mandula atakae pambana na Twalib Mchanjo na Fadhili Majia atakae menyana na Ally Mahiyo na Mustapha Doto atapambana na Hashimu Mjeshi mapambano yote ya utangulizi itakuwa ni ya raundi sita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2013

    du!!!! iko kisehemu cha mazoezi ni mgogoro tosha!!!!!

    ReplyDelete
  2. Du !! siyo mchezo ! hiyo sehemu ya kujiandaa na huo mpambano mbona imechoka sanaaaa....itabidi turudi bongo tuwaonyeshe namana ya kutengeneza boxing gym ya kisasa..hayas mambo ya usanii sanii hayatufikishi popote..sasa bondia kama huyu hata mahala pake pa kuishi na lishe yake itakuwa sio mzuri..poleni wanamichezo ktk kuwa na mazingira magumu..hadi hilo gurudumu nalo limechokaaa !!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2013

    Kweli michezo Tanzania tuna hali mbaya sana, Hebu tazama vifaa na mazingira wanaofanyia mazoezi wanamichezo wetu.

    Halafu hapa usikute ndio anazima moto, kapiga kambi siku moja au mbili hivi. duuuuuuuuuuuuh.







    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 29, 2013

    Don`t judge a book by its cover.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...