Afisa wa Bunge Ndg. Christopher Kanonyele akifafanua kwa wananchi majukumu ya msingi ya Bunge kama yalivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwal Nyerere.
Mwananchi akisikiliza kwa hisia maelezo kuhusu siwa ya Bunge na umuhimu wake katika vikao vya Bunge, kwenye maonesho ya sabasaba.
Afisa Habari wa Bunge Prosper Minja akifafanua hatua kwa hatua namna miswada inavyowasilishwa Bungeni hadi inapokuwa sheria kwa mwananchi aliyetembelea Banda la Bunge wakati wa Maonesho ya Sabasaba.
Wananchi wakifuatilia kwa makini maelezo ya picha za waliowahi kuwa maspika wa Bunge tangu kuanza kwake lilikiwa baraza la kutunga sheria mwaka 1926 kutoka kwa afisa wa Bunge Ndg. Ismail Jimrodger.
Muonekano wa Banda la Bunge kwa nje katika viwanja vya sabasaba. Picha zote na Owen Mwandumbya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2013

    Owen umeshindwa kuondoa hiyo ngazi katika picha ya chini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...