Ofisa wa Emirates Bi Lubna (kati) akiwa na baadhi ya wadau waliofika katika futari hiyo
Meneja wa Emirates katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Ustaadh Aboubakar Jumaa (kulia) akiwa na wadau waalikwa katika futari hiyo
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
wewe sheikh issa michuzi wakati mwingine sio vibaya nawewe ukapiga kanzu sehemu kama hizo usijisahau sana wewe ni issa
ReplyDeleteAsalam alaykum.
ReplyDeleteKwani ninani amesema kama kanzu ndio inayo mfanya mtu kuwa muislam?
Alaykum Salaam!
ReplyDeleteNaam Mdau wa Pili umenena, hii imekuwa ni tabia MBAYA SANA ya wengi wetu mfano unapo msalimia mtu ukiwa hujavaa Kofia ya ''Bargashia'' au Kanzu kwa kumpa 'Assalam Aykum' yeye inawezekana kabisa atanyamaza ama ataitikia kwa kejeli sana kama mojawapo ya hivi hapa chini.
1.MSALIMIAJI:''Assalam Alaykum''
MWITIKIAJI ''Salaaaaam'' !
2.MSALIMIAJI: ''Assalam Alaykum''
MWITIKIAJI ''Nini khabar'' !
3.MSALIMIAJI: ''Assalam Alaykum''
MWITIKIAJI ''Khaifa khabar'' !
4.MSALIMIAJI: ''Assalam Alaykum''
MWITIKIAJI ''Msalaaaam'' !
5.MSALIMIAJI: ''Assalam Alaykum''
MWITIKIAJI ''Vipi hali'' ?
Jamani SALAMU ni MOJA YA IBADA KUBWA SANA KAMA ITAITIKIWA KWA NAMNA INAVYOSTAHILI.
Hata Salamu inkuwa tabu?, inakuwa kama mtu ukiitikia sawasawa labda kama ulikuwa na LAKI MOJA mfukoni utakuta ELFU KUMI imepungua kwa kuitikia vyama salamu?
Tunakwenda wapi?
Ni muhimu tuchukue Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan kama Mafunzo ya kujirekebisha tabia hizi chafu kama KUWATATHIMINI WATU KWA MAVAZI
Mfano Ankal amevaa vazi zuri tu la Kistaaarabu kuna tatizo gani hapo?
Mfano unaposalimiwa ukiitikia vizuri kuna tatizo gani hapo?
TUBADILIKE!
Namuunga Mkono Mdau wa 2 Mdau,
ReplyDeleteUislamu wa mtu hautathiminiwi kwa kuvaa Kanzu peke yake, Kuwa na ndevu nyingi,kuweka HINA kwenye madevu ama kuvaa Kibandiko peke yake,
Imani ni Nafsi ya mtu, ungetoa dosari ya vazi kama vazi lingekuwa sio la stara.
Lakini hiyo aliyovaa Abkali hapo inakubalika hata kuendeshea Ibada.
Ankal yupo na Suti yake ya Kazini Serikalini Wajameni!
ReplyDeleteSasa mnafikiri kule Serikalini Ofisi Kuu wanavaa nguo zipi, naye inawezekana ametokea Ofisini moja kwa moja hadi kwenye Futari?
Mnajuaje, labda pale nyumbani akina Selah walikuwa wanaandaa futari huku Kanzu ilikuwa ingali sandukuni na haijapigwa pasi?
Mdau wa Pili juu kazi tunayo na ndugu zetu pmoja na Mdau huyo wa Kwanza juu wanaojiona wao ndio Waisilamu safi zaidi kuliko wengine.
ReplyDeleteZaidi aniyetoa kasoro kwa kutovaliwa kwa vazi la Kanzu, pana wale Maulamaa wetu wanapo salimiwa ASSALAM AALYKUM!, wao hujibu kwa Staili ya Passport size ALAYKUM!
Jamani, jamani, jamani, acheni mchezo ktk Dini ya Mwenyezi, hayo ya uitikiaji wa harau namna hiyo amefundisha Nabii gani?
Hivi ndivyo Mtume alitufundisha uitikiaji wa salamu kwa nusu mkate kama hivyo?