Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Kulia) akishuhudia Balazo wa China hapa nchini Balozi Lu Youging akiweka sahihi katika hati ya makabidhiano ya Uwanja wa Taifa.Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga(Kushoto) akitia sahihi katika hati ya makabidhiano ya uwanja wa Taifa,kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Habib Mkwizu.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Katikati) akishuhudia Balazo wa China hapa nchini Balozi Lu Youging akibadilishana hati ya makabidhiano ya Uwanja wa Taifa na Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga (Kulia).
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Utumishi Habib Mkwizu (Kushoto) akifafanua jambo kwa baadhi ya viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya sherehe ya makabidhiano ya Uwanja kukamalizika.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Assah Mwambene (Kulia) akizungumza akibadilishana mawazo na Katibu Mtendaji wa TFF Angetile Oseah walipokutana katika sherehe za makabidhiano ya Uwanja wa Taifa jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangaraka (kulia) akipokea Ufunguo wa mfano kutoka kwa Balazo wa China hapa nchini Balozi Lu Youging kuashiria kukabidhiwa rasmi kwa Uwanja wa Taifa.PICHA ZOTE NA FRANK SHIJA - MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2013

    Balazo, ni neno jipya la kiswahili?
    Naomba kujua ndugu mwandishi!
    Sina zaidi ni hilo tu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2013

    HONGERENI TANZANIA NA TUNAWASHUKURU SANA SERIKALI YA CHINA

    SASA KAZI KWAKO WAZIRI, UWANJA HUO UMEKABIDHIWA SAAAAFI KABISA, CJUI UTAKUAJE BAADA YA MIAKA MIWILI IJAYO, JE UTAKUA KAMA ULIVYO??KUKUSANYA TU PESA BILA KUKARABATI???

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 04, 2013

    Nashauri serikari itoe tenda kwa kampuni itakayoweza kuendesha huo uwanja kwa kuangalia kampuni itakayoweza kuendesha kwa faida na kutunza uwanja vizuri.
    Bila kufanya hivyo uwanja utachakaa mara mmoja na utakuwa sio endelevu hawaweza kutengeneza na kuendelea kuufanya wa kisasa kwa ku up to date kila mara.Facility Management company itaweza kufanya kazi vizuri.
    Ushauri wangu huu ni wa bure mimi ni Mtanzania naishi UK. Kwa ushauri zaidi wasiliana na mimi kupitia email: tanzaniauk@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 04, 2013

    Brother Misupu!
    Mimi nashauri Serikali waanzishe AGENCY au AUTHORITY ya kusimamia,kuendesha na kuendeleza viwanja vya michezo vikubwa (vile vidogo viwe chini ya halmashauri za maeneo husika) Mamlaka/Wakala hiyo iitwe STADIUMS MANAGEMENT AGENCY OF TANZANIA/TANGANYIKA.(SMAT)itahusika na viwanja kama huu mkuu wa taifa na ndipo yatakapo kuwa makao makuu ya Wakala, viwanja vya mikoani ni kama kirumba - mwanza, samora -iringa, jamhuri - dodoma, jamhuri - morogoro, mkwakwani - tanga, majimaji - ruvuma, ali h. mwinyi - tabora, abeid - arusha, sokoine - mbeya na shamba la bibi - dar.Wakala hii ianze kwa kuendeshwa kwa ruzuku ya serikali ya asilimia 80 na baadaye isimame yenyewe kwa kujiendesha bila ruzuku. mapato yake, pamoja na mgao wa viingilio, kuwe na miradi ya maduka, mahoteli, huduma mbalimbali kuzunguka eneo la viwanja, kukodisha kumbi na viwanja kwa sherehe, mikutano na matamasha, VIWANJA VIONDOLEWE KWENYE MIKONO YA CHAMA VIWE VYA SERIKALI KUPITIA WAKALA/MAMLAKA/SHIRIKA LA SERIKALI. ASANTE SANA

    ReplyDelete
  5. Mikausho MikaliJuly 04, 2013

    mnaushauri mnapoteza muda wenu bure.Wahusika wanayajua mnayosema lakini kwa hulka ya watz hapa ndo wakati wa kuneemeka.Tujiulize kuna tabu gani kuweka namba kwenye viti ? Ulaji tu

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 04, 2013

    WAMKABIDHI AZAM GROUP, KWA SASA NDIYO KAMPUNI INAYOTOA HUDUMA NZURI TANZANIA. ZANZIBAR WANAJUA NINI KAFANYA PALE BANDARINI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...