Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba,
atakutana na Wanahabari kesho, Ijumaa, Julai 5, 2013, kuanzia saa 4:00
asubuhi, katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume uliopo katika Ofisi za Tume,
Mtaa wa Ohio, jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo, pamoja na mambo mengine, Jaji
Warioba atazungumzia mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya kujadili Rasimu
ya Katiba itakayofanyika katika kila halmashauri ya wilaya. Mikutano
hiyo itaanza hivi karibuni.
Nyote mnakaribishwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...