Mahmoud Ahmad Arusha
MTU mmoja anaedaiwa kuwa ni Jambazi afariki katika majibishano ya silaha na polisi katika tukio
tofauti la kujibishana risasi na askari wa jeshi la polisi baada ya
kumfyatulia askari risasi na kumkosa huko maeneo ya Sokon 1 jijini hapa
jana majira ya jioni.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi
mkoani hapa Kamishna msaidizi wa polisi Liberatus Sabas alisema kuwa
mnamo majira ya saa11;15 huko mtaa wa Onjaftian jeshi hilo lilifanikiwa
kumuuwa baada ya majibishano ya risasi na askari wa jeshi hilo jambazi
sugu aliyefahamika kwa jina la Lembris Taiko au kwa majina mengine
doctor mbushii,general mwarusha, mwenye umri wa miaka32-35 mkazi wa
sokon 1 jijini hapa.
Kamanda alisema kuwa awali
walipata taarifa kwa wasamaria wema kuwa kuna watu3 wanaosadikiwa
majambazi na kufuatilia maeneo ya tukio na kuizingira nyumba
walipojaribu kuingia ndani na kuwataka watu wote kujisalimisha ghafla
risasi zilianza kutoka ndani kupitia ukutani na kumkosa askari hali
iliyowalazimu askari kujibu mapigo na kufanikiwa kumuua jambazi huyo.
Sabas
alisema kuwa uchunguzi uliofanya na askari wa jeshi hilo umebaini kuwa
ni jambazi sugu huyo alikuwa akitafuta na jeshi hilo na akishiriki
kwenye matukio ya ujambazi maeneo mbali mbali ikiwemo Arusha,Kilimanjaro
na Dar es salaam na alikutwa akiwa na bastola mmoja,aina ya bereta
iliyofutwa namba risasi moja chemba,ganda moja la risasi
iliyofyatuliwa,risasi 3za bunduki aina ya shortgun,na funguo mbali mbali
26 na mordem ya kampuni ya Airtel.
“Jambazi huyu
alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na jeshi letu kwa kushiriki kwenye
matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha za moto tukio ambalo
lilitokea28\08\2012 huko maeneo ya olasiti jijini hapa ambapo walipora
bastola yenye no.T0620-11J00491 aina ya tisas”alisema kamada sabas.
Katika
tukio lingine jambazi huyo alijeruhiwa mguuni akafaniwa kutoroka lakini
jeshi la polisi lilifanikiwa kumua jambazi aliefahamika kwa jina la
peter Toshi katika majibizano hayo jambazi huyo alikutwa na bastola aina
tisas inayoaminiwa kuwa ndio ilioporwa ikiwa imefutwa namba zake.
Kamanda sabas alisema kuwa kutoka eneo la tukio
anabainisha kuwa mmiliki wa nyumba aliokuwa jambazi huyo anaefahamika
kwa jina moja la Swalehe au baba Amiri ambaye hakuwepo wakati wa tukio
hili jitihada za kumtafuta zinafanyika ili aweza kuhojiwa juu ya
uhusiano wao na jambazi aliyeuwa na wapangaji wengine kwenye nyumba hiyo
kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi.
Hata hivyo
mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya mount meru
kwa uchunguzi zaidi na juhudi za kuasaka majmbazi wengine badao
zinaendelea kufanyika.
Iwe majambazi kweli lakini, isiwe kama ule mwimbo wa mrisho mpoto.
ReplyDelete