Na. Luppy Kunga’lo Polisi Dodoma
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu wawili wenye asilia ya kiarabu na watanzania watatu kwa tuhuma za kufanya utapeli na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu katika vituo vya kuuzia mafuta (sheli) na maduka ya kubadilishia fedha.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Bw, David Misime alisema Tukio hilo lilitokea juzi katika Sheli ya Camel Iliyopo karibu na Chuo Cha Mipango katika manispaa ya Dodoma.
Kamanda Misime alisema watu hao walifika katika sheli hiyo ambapo kulikuwa na duka na kuagiza soda kisha baadae kutoa dola ya kimarekani ya USD 50, ambapo muuzaji aliwaambia kuwa habadilishi pesa, hivyo kuamua kumdanganya kuwa wanahitaji pesa ya kitanzania kwa ajili ya kwenda kuonyesha Misri kama sehemu ya maonyesho.
“Wateja hao waliomba wapatiwe noti za 10,000/= za zamani ili wao wampatie noti mpya za 10,000/=, muuzaji huyo alichambua noti za zamani zipatazo shilingi 470,000/= na kuwapa kisha wao kumwambia wanazotaka kumbadilishia ziko kwenye gari na kujifanya kwenda katika gari na matokeo yake waliondoka kwa kasi” alieleza Kamanda David Misime.
Mkuu huyo wa Polisi Mkoa wa Dodoma alisema baada ya watu hao kuondoka kwa kasi ndipo muuzaji huyo kugundua kwamba ameibiwa na kupiga simu Polisi ambao waliwasiliana na vituo vyote vya mjini na nje ya mji na kufanikiwa kuwakamata matapeli hao katika kituo/barrie ya Chanene liyopo wilayani Chamwino pori la Mtungutu.
Kamanda Misime aliwataja watuhumiwa hao waliokuwa wakitumia gari aina RAV 4 T. 872 CGE la rangi ya damu yam zee kuwa ni mwanamke Ahlam d/o Hassan, miaka hamsini mwarabu na mkazi wa Tanga, mwanaume Daoud Esam@Abdelgawad , miaka 39 , msudani dereva na mkazi wa misri ambaye alikuwa na passport ya kuiingia nchini tarehe 19/07/2013 na ana Visa ya kukaa Tanzania kwa muda wa Miezi mitatu.
Wengine ambao baada ya kuhojiwa, Kamanda alisema walikiri kufanya utapeli huo ni Matata Laurence, miaka (38) dereva na mkazi wa Gongo la Mboto, Rahma Mahamoud, miaka (26) Mkazi wa Dar es Salaam pamoja na Salehe Hamad Mnene , miaka 40 na mkazi wa Manzese Dar es salaam.
Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kwa wanachi kuwa makini na ya watu wanaofanya vitendo vya namna hii na kuwataka kutoa taarifa mapema pindi wanapotia shaka kwa watu wa aina hiyo, ili hatua za kuwadhibiti zichukuliwe mapema.
Majanga mbona Majangaaaa!
ReplyDeleteUle mtazamo wa kuwa kila mwenye gari ni mtu mwenye uwezo sasa unakwenda ukingoni.
Matapeli wanaburuza hadi mchuma wakitembea kwa kukaa lakini mkono kwenda kinywani bado ni shughuli pevu.
Mtu unafikia umri wa Miaka 50 lakini Mipango ya maisha huna, unaishi kwa plan finyu kama Utapeli?
Arobaini yao hiyo
ReplyDeletena mungu kajua kuwaumbua wao mwezi huu mtukufu bado wanatapeli jamani ndo wakome wameumbuliwa lool
ReplyDeleteLakini hivi watu wengine akili zao zinaakili kweli?mimi nadhani wafanyakazi woote walio sehemu zenye kupokea fedha taslimu,mfano kama huyu wa kituo cha mafuta, hawa wanaorusha fedha kupitia mitandao ya simu,masokoni,dukani na kwengineko wanapaswa kua na umakini sana wa kuweza kugundua hila za aina yoyote za matapeli,Mara nyingi unaposoma taarifa kama hizi ni rahisi sana kugundua ufahamu wa mhanga haiwezekani mtu akubadilishie badilishie maneno tena kuhusu fedha alafu bado tu usistuke?
ReplyDelete