Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawa Mhe. Pindi Hazara Chana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. William Ngeleja wakiendesha kikao cha kupokea maoni ya wadau mbalimbali kuhusu muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba sura ya 83(2012) katika Ofisi ya Bunge, Dar es Salaam, leo.
Wajumbe na wadau kutoka Asasi mbalimbali (zikiwemo WLAC, TAWLA, LHRC, TANLAP, TUCTA na TLS) waliohudhuria kikao hicho.
Mhe. Tundu Lisu, Mjumbe wa Kamati akitoa ufafanuzi wa vifungu vya sharia.
Mwanasheria wa Mtandao wa Utoaji wa Msaada wa Kisheria Bi. Sarah Mkenda (TANLAP) akiwasilisha mapendekezo ya Asasi yake.
Mjumbe wa Kamati Mhe. Nyambali Nyangwini akichangia wakati wa mjadala na wadau.
Mjumbe kutoka The Tanganyika Law Society (TLS) akiwasilisha mapendekezo ya Asasi hiyo.Picha na Prosper Minja - Bunge.


Mimi nikimuona Tundu Lisu kwenye mjadala wowote huwa na imani kuwa halitaharibika jambo.. Huyu jamaa huwa namuaminia sana . Serikali ingemtumia vizuri mambo yangenda sawia
ReplyDeleteIkiwa Tanganyika haipo imekufa hii Tanganyika lawa society inatokea wapi!
ReplyDelete