Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Luteni Kanali Lidwino Saimon Mgumba (kushoto) akimvisha cheo Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Iringa, Mrakibu Msaidizi wa jeshi hilo, Kennedy Komba katika hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji, jijini Dar es Salaam leo. Naibu Kamishna Mgumba aliwavisha vyeo maafisa hao kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Pius Makuru Nyambacha. Picha na Puyo Nzalayaimisi, Afisa Mahusiano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Makao Makuu.
Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Luteni Kanali Lidwino Saimon Mgumba akiwaasa maafisa wa jeshi hilo waliovishwa vyeo katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es Salaam leo. Mgumba aliwaasa maafisa hao kutumia vyema vyeo na madaraka waliyopewa kwa uhadilifu na kwa kuzingatia sheria. Naibu Kamishna Mgumba aliwavisha vyeo maafisa hao kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Pius Makuru Nyambacha. Picha na Puyo Nzalayaimisi, Afisa Mahusiano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Makao Makuu.
Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na askari wakimsikiliza kwa makini Naibu Kamishna wa jeshi hilo, Luteni Kanali Lidwino Saimon Mgumba wakati alipokuwa akiwaasa maafisa wa jeshi hilo waliovishwa vyeo katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es Salaam leo. Mgumba aliwaasa maafisa hao kutumia vyema vyeo na madaraka waliyopewa kwa uhadilifu na kwa kuzingatia sheria. Naibu Kamishna Mgumba aliwavisha vyeo maafisa hao kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Pius Makuru Nyambacha. Picha zote na Puyo Nzalayaimisi, Afisa Mahusiano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Makao Makuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2013

    duh haya majeshi!!! sijui. muda si mrefu tutakuwa na jeshi la uhamiaji, jeshi la wanyama pori, jeshi la mgambo. au mimi ndo sielewi maana ya jeshi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2013

    Na kweli Anonymous hapo juu huelewi , kama huna uelewa piga kimya fanya utafiti kwanza UHAMIAJI NA ZIMAMOTO ni vyombo ndani ya Wizara ya mambo ya ndani, ni aibu kwamba hata mpaka leo hii huelewi kuwa uhamiaji na zimamoto ni nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...