Omar Sykes enzi za Uhai wake.

Na Swahili TV
Familia ya  mwanafunzi mtanzania aliyeuwa mjini washington DC, marehemu Omary Sykes inatarajiwa kuingia nchini Marekani leo hii, swahili TV inaripoti. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu familia hiyo itaongozwa na baba wa marehemu bwana Adamu Sykes na baba mkubwa  wake bwana Ilyasa Sykes.

Marehemu ambaye alikuwa na  miaka 22,  ni mjukuu wa mpigania uhuru maarufu wa Tanzania mzee Kleist Abdulwakili sykes na  pia ni ndugu wa  msanii star wa bongo Flava Dully Sykes.

Omar  aliuawa kwa shambulio la risasi karibu na maeneo ya chuo anachosoma cha Howard University usiku wa alhamisi julai 4, 2013 akiwa na mwenziwe katika mtaa wa Fairmont North West, kwa mujibu wa Polisi Washington DC (MPDC)  na Polisi wa chuo hicho (HPD), watu wawili ndio wanaoshukiwa kuhusika na mauaji hayo.Wahusika bado hawajatiwa mbaroni.

Kwa mujibu wa habari za ndani za jeshi hilo la Polisi, kitengo maalum cha uchunguzi wa mauaji kilishaanza upelelezi mkali ukiongozwa na Bwana Gabriel Truby wa MPDC na wameieleza Swahili TV kuwa  licha ya upelelezi wanaoendelea nao wanaomba ushirikiano wa wananchi kwa ajili ya kufanikisha uchunguzi wao. Zawadi ya dola za Kimarekani 25,000 itatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa wauaji hao. 

Maripota wa Swahili TV wamefanikiwa kufanya mawasiliano na kitengo cha mauaji cha MPDC, Howard University Police  pamoja na familia ya marehemu Omar Sykes. Kwa mujibu wa maelezo yao  mwili wa marehemu bado upo hospitalini kwa ajili ya uchunguzi na swahili TV inaahidi kuwaletea habari zote zinazohusiana na upelelezi huu. 
Stay tuned kwa exclusive story.
Tembelea http://swahilitv.blogspot.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2013

    Howard university is one of the best universities .may his soul rest in peace Jamani so sad

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 09, 2013

    R.I.P Omar Sykes.

    Mungu amlaze mahali pema.
    wauaji watapatikana na
    sheria itachukuwa mkondo wake.
    Poleni ndugu na marafiki wote
    wa Adam na Ilyasa Sykes.

    mickey "mikidadi" Jones
    denmark

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 10, 2013

    Mungu ailaze pema peponi roho ya mwenzetu,pia awape nguvu ndugu wa marehemu.
    Mikidadi unajiita mickey jones??upo ulaya?
    Njechele.
    Sweden.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 10, 2013

    R.I.P Omar.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 10, 2013

    "Mama uchungu", "mama uchungu", mama ya mwanangu tumbo la udele linauma mno wee!!!! Pole mama mzazi, mungu akusitiri na machungu haya!!!!!! Poleni wafiwa!!! Inna Allah, wa inna Illaihi raji'uunn. Mola awape hekima na subira kwa mtihani huu!!! Inauma sana!!!!Poleni sanasana.!!!!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 10, 2013

    Pole sana wafiwa.

    Anony wa kwanza usichanganye Harvard na Howard.
    Howard iko Washington DC.
    Havard ni chuo kikuu cha kwanza kujengwa huko marekani.
    -Kilijengwa mwaka 1636
    -Ada yake ni dola 40,866
    -Student Faculty Ratio ni: 7:1
    -Ni private
    -Rate of acceptance ni asilimia 6.3
    -Kiko Cambridge, jimbo la Massachusetts.
    Asante mdau.

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJuly 10, 2013

      Howard ni one of the best .My mother went to Harvard and my husband graduated from Yale ok .Howard is the one of the best for minority .

      Delete
    2. AnonymousJuly 10, 2013

      MDAU umechrmka Howard is the best no one historical Kwenye black university .Nimecheki Wikipedia. Mayors ,congressman wengi wamegraduate hapo Bill Cosby . College private hiyo .wangapi wanaenda private USA ?

      Delete
  7. AnonymousJuly 10, 2013

    Dude, you better review your facts before criticizing Howard University. Yes, Howard University is indeed one of the best universities in the United States. Why do you feel the need to compare between Howard and Harvard? that is irrelevant and completely pointless since the initial message never mentioned anything about Harvard.

    R.I.P Omar Sykes.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 10, 2013

    wadau wa huko juu nisaidieni mimi mtanzania sijielewi, hivi harvard ni chuo cha waadventista wasabato? au ni nini?

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJuly 10, 2013

      Harvard ni Chuo kikubwa USA ila asilimia kubwa ni white na foreighner.Watu weusi inakuwa ngumu kuingia .Howard Pia ni Chuo kikubwa kwa weusi na foreigners na white Lazima uwe na akili

      Delete
  9. AnonymousJuly 10, 2013

    OLE WETU WANTANZANIA! sasa nyie mnabishania kuhusu vyuo vikuu baada ya kuangalia possibilities za uhalifu huo na kutoa pole kwa WAFIWA, WATANZANIA KWA MAMBO WASIOWAHUSU BANA, YAANI TUNAPENDA SANA KUANGALIA YA ULAYA NA MAREKANI, HAYA BASI NA WEWE GEUKA UWE MMAREKANI, YAANI KAZI HOJA ZISIZO NA MSINGI TU. WEWE INAKUSAIDIA NINI HOWARD VERSITY KUA BEST AU LAA, HEBU ANGALIENI YA KWETU NA KUZITUMA AKILI ZETU KWENYE UVUMBUZI SIO KUBISHANA KWA JITIHADA WALIZOFANYA WEZETU SIO MAHALI PAKE KWA LEO HII.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 10, 2013

    Watanzania, Majuu na Hapa nyumbani Darisalama.

    INGEFAA TUPITISHE KOFIA NA KUTOA CHOCHOTE KAMA RAMBI RAMBI AMA UBANI KAMA ILIVYO DESTURI ZETU,AMA KWA UCHACHE KUTOA POLE NA BURIANI KWA WAFIWA BADALA KUBISHANA KUHUSU MAREKANI NA UBORA WA VYUO VIKUU!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 10, 2013

    Mnaobisha kuhusu Vyuo Vikuu vya Marekani hapa Jamivi Msibani, napitisha KAPU LA MCHANGO WA RAMBIRAMBI KWA WAFIWA, NAOMBA MTOE CHOCHOTE BADALA YA KENDELEZA MABISHANO!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 10, 2013

    Watanzania tuache JILAZI tubadilike!

    Hivi jamani ni ustaarabu kubishana kuhusu ubora wa Vyuo vya Marekani Msibani?

    Hapa ndio utakapothibitisha jinsi Watzania tusivyopendana na wengi tulivyo na wivu.

    Muogopeni Mwenyezi tumo ndani ya Mfungo wa Ramadhani.

    Angalieni BILA AIBU,HAYA WALA SONI, mnajadili hali ya uwezekano wa Marehemu kwa nini alisoma chuo chenye hadhi ya juu Marekani, sasa hiyo si ndio Jilazi ?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 10, 2013

    Eti nini???...Wauaji wanafahamika lakini hawaja wekwa Nguvuni?

    Lohhh ama kweli Dunia sasa imekuwa ni Msitu kweli, yani Marekani na mshike mshike wenu wa Usalama lakini mambo ya namna hii bado yanafanyika na majibu yanakuwa yanachukua muda namna hii?

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 10, 2013

    Poleni sana kwa Msiba huo.Ni huhuzuni kubwa kwa kijana mwenzetu kukutwa na mkasa huo.Maombi yetu ni kwamba waliohusika wakamatwe na wafikishwe ktk vyombo vya sheria.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 11, 2013

    NAFUNGA MJADALA WA VYUO.
    ASENTENI.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 11, 2013

    1 – 18 of 18
    Anonymous said...
    Howard university is one of the best universities.

    Howard IS ONE OF THE BEST ....................sasa kuna ubishi gani, wewe July 10, 2013 Anonymous, acha kujifanya unajua...........

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...