Omar Sykes enzi za Uhai wake.
Na Swahili TV
Familia ya mwanafunzi mtanzania aliyeuwa mjini washington DC, marehemu Omary Sykes inatarajiwa kuingia nchini Marekani leo hii, swahili TV inaripoti. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu familia hiyo itaongozwa na baba wa marehemu bwana Adamu Sykes na baba mkubwa wake bwana Ilyasa Sykes.
Marehemu ambaye alikuwa na miaka 22, ni mjukuu wa mpigania uhuru maarufu wa Tanzania mzee Kleist Abdulwakili sykes na pia ni ndugu wa msanii star wa bongo Flava Dully Sykes.
Omar aliuawa kwa shambulio la risasi karibu na maeneo ya chuo anachosoma cha Howard University usiku wa alhamisi julai 4, 2013 akiwa na mwenziwe katika mtaa wa Fairmont North West, kwa mujibu wa Polisi Washington DC (MPDC) na Polisi wa chuo hicho (HPD), watu wawili ndio wanaoshukiwa kuhusika na mauaji hayo.Wahusika bado hawajatiwa mbaroni.
Kwa mujibu wa habari za ndani za jeshi hilo la Polisi, kitengo maalum cha uchunguzi wa mauaji kilishaanza upelelezi mkali ukiongozwa na Bwana Gabriel Truby wa MPDC na wameieleza Swahili TV kuwa licha ya upelelezi wanaoendelea nao wanaomba ushirikiano wa wananchi kwa ajili ya kufanikisha uchunguzi wao. Zawadi ya dola za Kimarekani 25,000 itatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa wauaji hao.
Maripota wa Swahili TV wamefanikiwa kufanya mawasiliano na kitengo cha mauaji cha MPDC, Howard University Police pamoja na familia ya marehemu Omar Sykes. Kwa mujibu wa maelezo yao mwili wa marehemu bado upo hospitalini kwa ajili ya uchunguzi na swahili TV inaahidi kuwaletea habari zote zinazohusiana na upelelezi huu.
Stay tuned kwa exclusive story.
Tembelea http://swahilitv. blogspot.com/
Stay tuned kwa exclusive story.
Tembelea http://swahilitv.
Howard university is one of the best universities .may his soul rest in peace Jamani so sad
ReplyDeleteR.I.P Omar Sykes.
ReplyDeleteMungu amlaze mahali pema.
wauaji watapatikana na
sheria itachukuwa mkondo wake.
Poleni ndugu na marafiki wote
wa Adam na Ilyasa Sykes.
mickey "mikidadi" Jones
denmark
Mungu ailaze pema peponi roho ya mwenzetu,pia awape nguvu ndugu wa marehemu.
ReplyDeleteMikidadi unajiita mickey jones??upo ulaya?
Njechele.
Sweden.
R.I.P Omar.
ReplyDelete"Mama uchungu", "mama uchungu", mama ya mwanangu tumbo la udele linauma mno wee!!!! Pole mama mzazi, mungu akusitiri na machungu haya!!!!!! Poleni wafiwa!!! Inna Allah, wa inna Illaihi raji'uunn. Mola awape hekima na subira kwa mtihani huu!!! Inauma sana!!!!Poleni sanasana.!!!!!!
ReplyDeletePole sana wafiwa.
ReplyDeleteAnony wa kwanza usichanganye Harvard na Howard.
Howard iko Washington DC.
Havard ni chuo kikuu cha kwanza kujengwa huko marekani.
-Kilijengwa mwaka 1636
-Ada yake ni dola 40,866
-Student Faculty Ratio ni: 7:1
-Ni private
-Rate of acceptance ni asilimia 6.3
-Kiko Cambridge, jimbo la Massachusetts.
Asante mdau.
Howard ni one of the best .My mother went to Harvard and my husband graduated from Yale ok .Howard is the one of the best for minority .
DeleteMDAU umechrmka Howard is the best no one historical Kwenye black university .Nimecheki Wikipedia. Mayors ,congressman wengi wamegraduate hapo Bill Cosby . College private hiyo .wangapi wanaenda private USA ?
DeleteDude, you better review your facts before criticizing Howard University. Yes, Howard University is indeed one of the best universities in the United States. Why do you feel the need to compare between Howard and Harvard? that is irrelevant and completely pointless since the initial message never mentioned anything about Harvard.
ReplyDeleteR.I.P Omar Sykes.
wadau wa huko juu nisaidieni mimi mtanzania sijielewi, hivi harvard ni chuo cha waadventista wasabato? au ni nini?
ReplyDeleteHarvard ni Chuo kikubwa USA ila asilimia kubwa ni white na foreighner.Watu weusi inakuwa ngumu kuingia .Howard Pia ni Chuo kikubwa kwa weusi na foreigners na white Lazima uwe na akili
DeleteOLE WETU WANTANZANIA! sasa nyie mnabishania kuhusu vyuo vikuu baada ya kuangalia possibilities za uhalifu huo na kutoa pole kwa WAFIWA, WATANZANIA KWA MAMBO WASIOWAHUSU BANA, YAANI TUNAPENDA SANA KUANGALIA YA ULAYA NA MAREKANI, HAYA BASI NA WEWE GEUKA UWE MMAREKANI, YAANI KAZI HOJA ZISIZO NA MSINGI TU. WEWE INAKUSAIDIA NINI HOWARD VERSITY KUA BEST AU LAA, HEBU ANGALIENI YA KWETU NA KUZITUMA AKILI ZETU KWENYE UVUMBUZI SIO KUBISHANA KWA JITIHADA WALIZOFANYA WEZETU SIO MAHALI PAKE KWA LEO HII.
ReplyDeleteWatanzania, Majuu na Hapa nyumbani Darisalama.
ReplyDeleteINGEFAA TUPITISHE KOFIA NA KUTOA CHOCHOTE KAMA RAMBI RAMBI AMA UBANI KAMA ILIVYO DESTURI ZETU,AMA KWA UCHACHE KUTOA POLE NA BURIANI KWA WAFIWA BADALA KUBISHANA KUHUSU MAREKANI NA UBORA WA VYUO VIKUU!
Mnaobisha kuhusu Vyuo Vikuu vya Marekani hapa Jamivi Msibani, napitisha KAPU LA MCHANGO WA RAMBIRAMBI KWA WAFIWA, NAOMBA MTOE CHOCHOTE BADALA YA KENDELEZA MABISHANO!
ReplyDeleteWatanzania tuache JILAZI tubadilike!
ReplyDeleteHivi jamani ni ustaarabu kubishana kuhusu ubora wa Vyuo vya Marekani Msibani?
Hapa ndio utakapothibitisha jinsi Watzania tusivyopendana na wengi tulivyo na wivu.
Muogopeni Mwenyezi tumo ndani ya Mfungo wa Ramadhani.
Angalieni BILA AIBU,HAYA WALA SONI, mnajadili hali ya uwezekano wa Marehemu kwa nini alisoma chuo chenye hadhi ya juu Marekani, sasa hiyo si ndio Jilazi ?
Eti nini???...Wauaji wanafahamika lakini hawaja wekwa Nguvuni?
ReplyDeleteLohhh ama kweli Dunia sasa imekuwa ni Msitu kweli, yani Marekani na mshike mshike wenu wa Usalama lakini mambo ya namna hii bado yanafanyika na majibu yanakuwa yanachukua muda namna hii?
Poleni sana kwa Msiba huo.Ni huhuzuni kubwa kwa kijana mwenzetu kukutwa na mkasa huo.Maombi yetu ni kwamba waliohusika wakamatwe na wafikishwe ktk vyombo vya sheria.
ReplyDeleteNAFUNGA MJADALA WA VYUO.
ReplyDeleteASENTENI.
1 – 18 of 18
ReplyDeleteAnonymous said...
Howard university is one of the best universities.
Howard IS ONE OF THE BEST ....................sasa kuna ubishi gani, wewe July 10, 2013 Anonymous, acha kujifanya unajua...........