Home
Unlabelled
KIJIWE CHA UGHAIBUNI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Nimeangalia mpaka dakika ya 7:41 nimechefuka na hoja hafifu na "booty licking, akata-esque" arguments. Mtu mweusi anatembea mitaa ya Florida, Mzungu anapiga simu Polisi.
ReplyDeleteMtu mweusi ambaye hakuwa na silaha anapigwa risasi; kisha waafrika wanaitetea "Justice system" iliyomwachia mzungu huru.
Hawa jamaa upeo wao kwenye hili sakata la Tryvon uko mdogo sana!!!
ReplyDeleteHawajagusa kabisa mambo ya msingi!!!
Nyinyi Wafrika umliokwenda kuishi USA ni watumwa na mnatumiwa kusema mambo wanayotaka Wazungu huko USA. Hapa UK hata silaha (hata kisu) huruhusiwa kutembea nazo wacha kujihami nazo. Ubaguzi upo na mahakama za USA zinongoza kwa ubaguzi. Je mnalionaje hili Zimmerman aliposema ameona kijana mweusi amekaa pale "hana kitu kizuri anachokisubiri" wache nende kumshughulikia. Mtu sio polisi kwanini aaze kukuhoji unachofanya? Jaribuni kuwa na akili sio mgeuke watumwa kutaka kupewa viza.
ReplyDeleteKila siku nilikuwa najiuliza kwanini wanugu (wamarekani weusi) hawawapendi waafrika. Hii video imeshajibu swali langu.
ReplyDeleteMkuu hapo juu, huwezi fananisha sheria za UK na USA. Hata hapa America, sehria za Floeida hazilingani na za New York. Kama UK huruhusiwi kutembea ha na kisu, sheria za majimbo mengi marecan zinaruhusu.
ReplyDeletePia, Zimmerman alikiuwa ni watch man wa ile community. Kwa hiyo akiona kitu chochote kipo na mashaka anareport. Ndio maan alipo muona Martin akasema kuna mtu anaoneka hapa kama yupo for "no good" Kumbuka ilikuwa usiku na Martin alikuwa kavaa "hood" mikono mirefu- sasa utajuaje kama ni mweusi au mweupe?
Inaonekana wachangiaji wengi hapo juu wanaiangalia kesi hii kulingana na uafrica na uzungu. Punguzeni munkali na angalieni kulingana na sheria
Nimeifatilia hii kesi kwa sehemu kubwa, kwa ufahamu wangu hii ni kesi ya kibaguzi asilimia 100%. Zimmerman aliambiwa asimfatilie Tryvon, lakini akapuuza na kumuua Tryvon. Kwa akili finyu ya Zimmerman mtu mweusi ni muovu, ndio maana alimuua. Majaji sita walioamua kesi hii yote ni weupe. Kura za awali zilifungana 3 walisema zimmerman(nimeandika herufi ndogo kwa makusudi) ana hatia na wengine 3 wakasema hana. Baada ya kura kurudiwa ndio wakasema kuwa zimmerman hana hatia. Uwezi ona kama majaji wangebalansi weupe na weusi- weusi ambao wanajua nini maana halisi ya kubaguliwa huyu zimmmerman angehukumiwa. Siku zingine mnapoweka mada jaribuni kupata walau wataalamu wa hiyo topic angalau wawili. With due respect hawa wanaojadili hapa hakuna chochote cha maana wanachoongelea juu ya hii kesi. Kilakshari
ReplyDeleteNakubaliana na wadau kuwa hii case imekaa ki-utata zaidi hebu angali rais wa marekani anasema nini afu na wewe unasema nini? Tafakari kwanza kabla ya kuzungumza
ReplyDeletehttp://www.bbc.co.uk/news/world-us-canada-23382880
Tatizo hapa ni kwamba hawa wana-kijiwe wameikuta marekani inaimba "Human rights" sasa wao wanadhania kwamba marekani ilivyo sasa ndiyo imekuwa hivi kwa karne kadhaa. Wanugu wanaijua historia yao kuliko hawa wanakijiwe, na haiwezekani kuiangalia historia ya marekani pasipo kuangalia rangi ya ngozi ya mwanadamu. Hawa wanaomteteaZimmerman (ingawa siwafahamu) lakini kwa uzoefu wangu naweza kusema kwamba aidha wote au wengi wao wana wanawake wa kizungu. Waafrika wenye wanawake wa kizungu ndiyo wanavyokuwa namna hii. They live their lives up to someone else's expectations. Eventually wanakuwa namna hii.
ReplyDeleteTena kuna huyu mwingine anasema "watu weusi waache kupigania haki zao kwa kutumia rangi"? Ebo??? are you for real? in america? Wanugu wameishi na ubaguzi wa rangi kwa miaka karibu 500. Leo wewe Mmatumbi upo marekani kwa miaka 10 tuu; unataka watu wajisahaulishe maumivu yao ya miaka 500 kwa sababu ya "american dream" yako wewe ya miaka 10.?
Swali la kujiuliza hapa; jee huyu 1. Zimmermann angeweza kumpiga risasi mtoto wa kizungu asiye na silaha? Au watoto wa kizungu wao hawavai hoods?
2. Jee, kama angemuua mtoto wa kizungu, Zimmerman angeachiwa?
Mtu anampiga risasi mtu ambaye halikua hana silaha huyo ni muuaji tu.
ReplyDeleteHawa jamaa wa "kijiwe cha ughaibuni" naweza nikawatafsiri kwa neno moja tu NAIVE!! Na kwa kweli hawastahili kabisa kupewa attention yetu, maana ni wapotoshaji wakubwa wa hali halisi.
ReplyDeleteMbona O.J Simpson aliachiwa huru baada ya kushitakiwa kuwa alimuua mkewe mzungu na mtoto ?Je hapo weusi walibaguliwa?
ReplyDeleteWewe umakuja na OJ Simpson. Simpson hakuachiwa huru. Washitaki hawakuweza kuthibitisha kama Simpson ndiye aliyeua.
ReplyDelete