Kikosi cha Timu ya Taifa (Taifa Stars) kikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebe nchini Uganda jioni ya leo,tayari kwa mtanange wa marudiano na timu ya Taifa ya nchi hiyo utakaopigwa mwishoni mwa wiki hii.
Kikosi cha Taifa Stars kikiwa uwanja wa ndege wa Mwanza kikisubiri usafiri kilikutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye naye alitua hapo kwa muda akielekea Bukoba kwa ziara ya siku sita mkoani Kagera
Rais Kikwete akisalimiana na wachezaji wa Taifa Stars jijini Mwanza
Rais Kikwete akiwatakia Taifa Stars kila la heri katika mchezo wao wa marudiano
hivi jamani mbona baadhi ya watu sio wastaarabu au niseme ndio UJINGA wa simu kweli unasalimiana na rais kiongozi wa nchi uko na kijisimu cha mchina mkononi
ReplyDeletekweli hii heshima yaani hata baba yako kumpa mkono na simu mkononi ni dharau kubwa au mtu yeyote yule unaemuheshimu nashangaa sana sisi watanzania tuliowengi sana tunaulimbukeni sana wa simu
utamkuta mtu anafanya kitu cha maana sana ila simu iko mkononi jamani simu kweli niyamkononi ila sio wakati wote tubadilikeni jamani watanzania
Naungana na Mdau wa Kwanza:
ReplyDeleteSimu Mikononi ni tabia ya Ubwege sana!!!
Simu kitu gani?
Jambo lingine pana ile tabia ya mtu muda wooote yupo buzy na simu yake, unakuta anapekua ktk fone book na kupiga simu bila umuhimu wowote au anatumia muda mwingi ku-chat bila mpango wowote.
Tanzania ni muhimu tukabadilika kwa kuacha hulka za ajabu ajabu, hubu tazameni unafiukia kipindi unasalimiana na Raisi wa nchi yako lakini simu bado ipo mkononi!!!
Taifa Stars ni wakati wenu sasa kilpa Fadhila!!!
ReplyDeleteRaisi Jakaya Mrisho Kikwete ameshawabeba saana kwa Ufadhili wa Michezo lakini bado hambebeki, jamani hii sasa ni aibu.
Hebu tumieni Mechi hii angalau mumfanye JK afarijike kidogo angalau kwa hasara kubwa alizotumi kwenu lakini hatusongi mbele kila uchao.
Nakubaliana na mdau Stars wajitume katika mechi hii ya pili na Cranes-uganda washinde mchezo huu muhimu saana,wakifungwa tena basi kama nilivyosema mwanzoni kufanyike mabadiliko kuanzia kocha na wachezaji mapema,tunataka kuwaona wachezaji wanaocheza kwa maelewano ya ushindi katika mechi za kimataifa hatuwataki wachezaji wa majaribio kufuatana na majina au klabu wanazocheza katika ligi.
ReplyDeletemikidadi-denmark