Licha ya Taifa Stars kushindwa kufuzu kucheza katika mashindano ya CHAN mwakani baada ya kufungwa na Uganda Cranes 3-1, wadhamini wa Stars, Kilimanjaro Premium Lager wamesema hawajakata tama nab ado wana imani na timu nzima na kocha Kim Poulsen.
Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya Stars kuwasili, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema licha ya habari hizi kutokuwa njema kwa watanzania, ni vizuri kukubali matokeo na kuangalia picha kubwa na malengo ya muda mrefu.
“Ni vyema tukumbuke kuwa kwenye mpira kuna kushinda na kushindwa,” alisema Bw Kavishe na kuongeza, “Tunapenda kuwahakikishia watanzania kuwa sisi kama wadhamini hatujakata tama na bado tuna imani na timu hii na kocha Kim Poulsen kwa hivyo tunawaomba watanzania wasife moyo.”
Alisema wakati walipoanza kuidhamini Taifa Stars mwezi Mei mwaka jana na kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa mwaka, kwa muda wa miaka mitano, walikuwa na malengo kadhaa ikiwemo kuinua hadhi ya Timu ya Taifa, kuhakikisha wanaingia kambini kwa muda unaotakiwa, wanalipwa vizuri, wanakula na kulala vizuri na kusafiri vizuri.
“Tumejitahidi kufanya mambo haya kwani wachezaji sasa hivi wana DVD zenye maelezo yao, tumewapa suti mpya na za kisasa na pia tumewapa basi jipya la kisasa. Mambo haya yote pamoja na mambo wanayofundishwa na Mwalimu Kim Poulsen yamesaidia kuleta mabadiliko kwa timu ya Taifa,” alisema.
Alisema kuna mafanikio mazuri ya timu ya taifa ambayo watanzania lazima wayakumbuke kama kuzifunga timu kama Zambia, Cameroon, Morocco na Kenya .
Kwa mujibu wa Meneja huyo walipoanza udhamini Tanzania ilikuwa katika nafasi ya 145 kwa mujibu wa FIFA lakini sasa imesogea hadi 109. “Haya ni mafanikio makubwa kwani tumesogea hatua zaidi ya 40,” alisema.
Alisema safari ya mafanikio katika mpira ni ndefu na inahitaji uvumilivu wa hali ya juu na kuongeza kuwa Kocha Kim Poulsen anafanya kazi nzuri ya kuibua vijana.
“Kocha anahitaji kuungwa mkono na sisi sote kuanzia kwa TFF, sisi wadhamini na watanzania wote. Tunahitaji kuangalia picha kubwa,” alisema na kuongeza,”Nawaomba watanzania tuwe wazalendo wakati huu hii ni timu yetu na tunatakiwa kujivunia. Vyombo vya habari pia viwe mstari wa mbele kuonesha uzalendo.”
Alisema mechi dhidi ya Gambia itakayochezwa mwezi wa 9 ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia ni muhimu hata kama Tanzania haisongi mbele kwani itasaidia katika ngazi za FIFA.
Msithubutu kuwashonea suti tena!! Michezaji isiyojua kwanini ipo timu ya Taifa yenye tabia ya kususa susa ya nini? Haijitumi!!! Safari hii sio makocha wala nini, Ni yenyewe imetufungisha, ndio ilikuwa hajitumi lazima tufe moyo!!!
ReplyDeleteKama mnawalipa pesa-mbili watajituma je? Hata wewe uliko usingejituma kama ungelipwa hivyo
ReplyDeleteHakuna njia ya mkato kwenye mpira lazima mfufue mashindano ya shule za msingi ya michezo yote huko ndio wanatoka vijana wenye vipaji na mashindano ya shule za secondary ya michezo yote kama ilivyokuwa zamani kwenye miaka ya 1970 .lakini kwa kuwajaza mahela na makocha wazuri haisaidii kwa sababu msingi wao sio mzuri wachezaji ni sawa na mwanafunzi wa shule ya msingi unampleka chuo kikuu eti kwa sababu alikuwa mzuri na kule kuna maprosa haiendi hivyo mnatakiwa muanzie chini hata ikichua miaka 10 mkawekeza kule chini makocha wazuri mtafanikiwa kwani tanzania kuna wachezaji wazuri na hata wanariyadha wazuri
ReplyDeleteToo much emphasis on Yanga and Simba, that is where bongo football starts and ends.
ReplyDeleteKazi kubeba mibag mikubwa. Kushoo off tuu!! Mpira hakuna. Ubishoo tuu!!!!!! Halafu mnataka mkacheze nje thubutuu!!!!! Mpira wa ndani umekushindeni mtauweza wa nje!!!!!!
ReplyDeleteMuonekano wao unaonyesha kukata tamaa.
ReplyDeletewape msosi na malipo ya ukweli KAZO ITAENDA
michezaji mijinga na mivivu, mpira unatoka langoni kwao, unagonga kibendera unarudi uwanjani, washambuliaji wa uganda wanakimbilia, wachezaji wa stars haiwahusu? Hata kama wanalipwa pesambili hawajui kuwa wakionyesha juhudi wanaweza chukuliwa na wanaolipa pesa milioni, Samata alikuwa analipwa bei gani hapa mpaka akawa na juhudi iliyofanya TP MAZEMBE wamuone? Samata na Ulimwengu wakijachezea Stars huwa wanalipwa kiasi gani mpaka wawe na juhudi na hiyo mipumbavu mingine isiwe na juhudi? tuache utamaduni wa kutetea wazembe.
ReplyDeleteSio siri, ninyi Stars inji ingekuwa yangu, ningeliwachapa bakora bila nguo, maana hamsikii hata mkifundishwa na kocha toka mbinguni ni sawa na kuti maji kwenye gunia, mnakula pesa za sponsors tu hakuna faida ya kuwa na timu yenye kigugumizi, ni bora tukate mshindano yote warudi kucheza mchangani, watu ubishoo mwingi wakati hakuna stamina wala nini.
ReplyDeletemimi
Mfurukutwa wa Michezo
JKL
Hawa wachezaji wetu ni wazembe na ni wajinga sana! Wanatakiwa kuelewa kuwa sie mashabiki tunaumia sana kuona ujinga wao wanaofanya uwanjani. Vijana endeleeni na ujinga wenu huo muone kama mtakuja kutoka, mtaishia hivyohivyo na ubishoo wenu wa kishamba. Wenzenu wanajenga heshima kwakuheshimu kazi zao. Kuna watu wamefanyia kazi uwezo wao kwa kufanya mazoezi ya ziada kama akina Ronald (physic yake), Bekham (kupiga Cross), Ronadinyo (ku umudu mpira- control. Ila vijana wetu wa Taifa Stars ni kula ughali na mandondo tu. Mhe. Mkapa amewajengea uwanja mzuri, Mhe. Dr. J.K kawaletea walimu wazuri, nini sasa mnataka???? Endeleleni na kuvaa milegezo mkidhani huo ndiop ujanja kumbe ushamba tu. Mie nahasira nao hao, achaa tu.
ReplyDeleteNilikwisha zungumza mwanzoni hatuhitaji mwalimu toka nje kwa sasa wakati hatuna timu nzuri ya kuelewana na kucheza kama timu ya maelewano turudi mwanzoni kuanza upya kuipanga timu ya Taifa Stars
ReplyDeletena pendekezo kubwa ni ADOLF apewe nafasi ya kujiandaa na wachezaji wapya vijana chini ya umri 25. Kim poulsen tumpe shukrani zetu na kurudi kuwakilisha timu zingine za ligi ya Denmark,wasaidizi wake wasaidie kuimalisha "academy school" za mpira na muundo wa ligi kabambe ya taifa subira tumeivuta muda mrefu tunachotaka mabadiliko.
mikidadi-denmark