Kongamano la Uongozi linaloandaliwa na Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) limefanyika leo katika hoteli ya Serena na kuhudhuriwa na Jumla ya washiriki wapatao 150, ambao ni viongozi mbalimbali wa sasa na wastaafu walishiriki katika kongamano hilo. Viongozi hao ni pamoja na Wah. Mawaziri Wakuu Wastaafu; Baadhi ya Wah. Mawaziri Wastaafu; Wah. Wabunge; Wenyeviti wa Kamati; Makatibu Wakuu Viongozi Wastaafu; Baadhi ya Wakuu wa Mikoa; Baadhi ya Viongozi wa Halmashauri; Wenyeviti wa Baadhi ya Taasisi za Umma; Watendaji Wakuu wa Baadhi ya Taasisi za Umma; Viongozi Kutoka Sekta Binafsi; Viongozi wa Asasi za Kiraia; Viongozi wa Dini and Wasomi na Watafiti.

Mgeni rasmi katika Kongamano hilo alikuwa Mh. Mizengo P. Pinda, Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mh. Pius Msekwa, Spika Mstaafu wa Bunge la Muungano, Tanzania ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa kongamano hilo pia lilipata nafasi ya kuwatuza wanafunzi waliofanya vizuri katika shindano la kuandika insha kuhusu uongozi bora na kuwashirikisha wanafunzi toka nchi zote za Afrika Mashariki huku Redemptor Benedict, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akiibuka mshindi.

Kongamano la uongozi mwaka huu liliongozwa na spika mstaafu, Pius Msekwa ambaye ndiye alimkaribisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda na watoa mada wengine ambao ni viongozi wa kitaifa, wastaafu na wale wa taasisi binafsi ambao wote walielezea changamoto zinazoikabili Tanzania katika uongozi na namna uongozi unavyopaswa kwenda na mabadiliko yanayojitokeza ikiwemo yale ya kisayansi na teknolojia.

Mgeni rasmi katika Kongamano la Uongozi, Waziri Mkuu Mizengo panda katika meza kuu.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua rasmi Kongamano la Uongozi liliofanyika Hoteli ya Serena jijini.

Mkongwe wa siasa nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwilu alikuwa mmoja wa wachangiaji

Mheshimiwa James Mbatia katika kongamano la uongozi

Katibu mkuu wa CCM (Mstaafu) Wilson Mukama alikuwa mmoja ya waliotoa changamoto kwa viongozi wa sasa na wajao

Mbunge wa zamani, Getrude Mongella alipata nafasi ya kuchangia mada katika kongamano kuelezea uzoefu wake

Alieibuka kidedea katika shindano la uandishi wa insha, Redemptor Benedict akipongezwa na Waziri Mku, Mizengo Pinda na kukabidhiwa cheti cha ushiriki.

Mshindi wa pili Joan Wanjiku Gichomo akisoma insha yake mbele ya washiriki wa kongamano la uongozi.

Viongozi mbalimbali walioshiriki katika Kongamano la Uongozi lilioandaliwa na Uongozi Institute katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2013

    Hiki kiazazi cha mlegezo hakijui matumizi ya "r", kwenye "r" wanaweka "l" and vice versa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2013

    wazungu wana kitu hichi cha ku use mind game na kinafanya kazi kweli hizi kongamano najiuliza kila pembe ya nchi yetu ni kwa manufaa ya nani? na raia wa kawaida mlalahoi ananufaika je na je ataambiwa juu ya hizi kongamano?tanzania ya leo si ya jana na kila kinachotokea ulimwenguni kina tu involved na sisi na sisi ni taifa changa na hata tukifanya au kutaka kuwa katika 21 century si rahisi kabisa naona pesa za umma zina liwa vibaya sana na kupotea bila hata ya kumnufaisha mlalahoi mkulima kijijini ukiaka maisha siku hizi uwe mwanasiasa ndo kilichobakia is such a sad sad sad thing but life goes on and good is great

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...