Sekoutoure
Khalifa Mndeme (24 Julai 1965 – 10 Julai, 2011)
Tarehe
10 Julai, 2011 Sekoutoure ‘Toure’
Khalifa mzawa wa Usangi, Wilaya ya Mwanga, mkazi wa Kunduchi-Mtongani, Dar
es Salaam, aliaga dunia katika Hospitali ya Apollo, nchini India.
Jamii
ilitoa msaada mkubwa tangu pale Toure alipolazwa Hospitali ya Aga Khan mwishoni
mwa Juni, baadaye akahamishiwa Taasisi ya MOI (Muhimbili) na kisha kupelekwa
India kwa uchunguzi zaidi na matibabu, hadi alipofariki. Tuliendelea kupata
ushirikiano wenu hadi mwili wa Toure ukarejeshwa Dar toka India tarehe 13 Julai
na hatimaye kusafirishwa kwenda Usangi–Ngujini kwa mazishi, Ijumaa, trh 15
Julai, 2011.
Familia
ya Sultani na Omari Muyanza ya Usangi Mwanga, ya Hemedi Mwamtemi ya Lushoto na ile ya Toure (mjane Halima H. Mwamtemi, wanawe Khalifa (18), Hemedi (15) na Bi Hafsa
“Doctor” (8) walifarijika mno kwa upendo na ushirikiano wa ninyi ndugu,
jamaa, majirani na marafiki.
Leo
tarehe 10.07.2013, Bw. Sekoutoure ‘Toure’ Khalifa ametimiza
miaka miwili (2) tangu alipofariki.
Familia
inafarijika sana kwa upendo na ushirikiano unaoonyeshwa na ndugu, jamaa na
marafiki tangu mpendwa wetu alipotutoka hadi leo. Tunawashukuru sana na
tunawaomba muendelee na upendo mlionao kwetu. Pia, tunawaomba muendelee
kumuombea ndugu yetu kwa Allah.
Toure;
ni kweli kwamba umetutoka kimwili, lakini utabaki ndani ya mioyo yetu daima.
Upendo, ucheshi, hekima na busara zako zitabaki kama dira na changamoto ya
kuwania ubora kwa sote ulotuacha nyuma.
“INNA
LILLAH wa Ina ILLAYH RAJ’UNN – Kwa Mola tumetoka na Kwake tutarejea.” - Al
Quran, Sura 6:128
MOLA
AILAZE ROHO YA SEKOUTOURE MAHALI PEMA PEPONI - AMINA.
Shukran
RIP Sekoutore, nilifanya kazi na huyu mpendwa CRDB LUmumba miaka ya 1993 hadi 94.
ReplyDelete