Karibu katika mahojiano baina ya Jamii Production na waTanzania wanaomiliki Chuo cha Uuguzi cha Kansas Ndg Michael Katunzi na Ndg Robert Otto.
Katika mahojiano haya, wanaeleza mambo mbalimbali ikiwemo walipopata na walivyopata wazo la kuanzisha chuo hiki, walivyoanzisha na walipo hivi sasa, changamoto walizokutana nazo kuanzia kuanzisha mpaka kilipo sasa, mafanikio yao na ya chuo chao pamoja na mipango yao juu ya chuo hicho kilicho katika nafasi za juu miongoni mwa vyuo vya uuguzi jimboni humo.
Karibu uungane nasi

Wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi cha Kansas College of Nursing wakiwa darasani

Wafanyakazi wa Kansas College of Nursing

Wanafunzi wa Kansas College of Nursing

Wanafunzi wa Kansas College of Nursing

Mahojiano baina ya Jamii Production na waTanzania wanaomiliki Chuo cha Uuguzi cha Kansas Ndg Michael Katunzi na Ndg Robert Otto
Hongera wadau wa "Care homes US" kwa mafanikio. Miaka ya tisini mpaka elfu mbili kulifumka vyuo vya "Computing" huku Ughaibuni. Sasa vyuo hivi vingi vimefungwa kwa kukosa wanafunzi. Ushauri wa bure msijisahau na mafanikio mliyopata hivi sasa. Siri ya mafanikio ya nyanja ya elimu ni upatikanaji wa kazi.
ReplyDeleteHongereni sana je wanatoa course za level gani? naweza kupata maelezo ya kupata nafasi?
ReplyDeleteHongereni sana. Wadau naomba kuuliza nataka kwenda kusoma chuo cha unesi USA je ni dollar ngapi kwa mwaka. Msiponde oooh mbona unaenda kusomea unesi sababu najua nifanyalo, mwenye jibu anisaidie tu.
ReplyDeleteAsanteni
Ankal
ReplyDeleteKwa kweli, hao waBongo wawili wamenifurahisha sana. Nilisikiliza hayo mahojiano yao, nikaishiwa nguvu kwa jinsi walivyo makini katika kujiwekea malengo na kuyafuatilia. Halafu wanajiamini kabisa, na uwezo wanao. Ni mfano wa kuigwa.
Nawaombea mafanikio zaidi na zaidi. Huwezi kujua, kesho na keshokutwa wanaweza wakafungua chuo au vyuo Tanzania, wakaineemesha nchi kwa uzoefu na elimu waliyo nao.