Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Yahya Msulwa (aliyesimama) akizungumza na Wajumbe a Baraza
la Katiba la Wilaya la Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara wakati wa
kufunga mkutano wa Baraza hilo jana Jumatatu (Julai 29, 2013). Kushoto ni Kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Babati Mjini, Bi.
Christina Mndeme (kushoto).
Mjumbe wa Baraza la Katiba la Hamshauri ya Mji wa Babati Mkoani
Manyara, Bi. Zainab Zubery akitoa Maoni yake kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya
iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika
ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo
Mjumbe wa Baraza la Katiba la Hamshauri ya Mji wa Babati Mkoani
Manyara, Mchungaji Wilson Ihucha akitoa
Maoni yake kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo
l
Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani
Manyara Bw. Yahya Ramadhani (kulia), akisoma nakala ya Rasimu ya Katiba Mpya
ilitolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa mkutano uliotishwa na Tume
katika Halmashauri hiyo
Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoani
Kilimanjaro, Bw. Bakari Mbaga akitoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya
iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika
ukumbi wa Chuo cha Ualimu Green Bird Wilayani humo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...