Wajumbe wa mkutano mkuu wa shirika lisilo la kiserikali
linaloshughulika na maswala ya jinsia na wanawake mkoani Kilimanjaro,
(KWIECO) wakifanya sala kabla ya kuanza kwa mkutano mku wa shirika
hilo.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali
linaloshughulika na maswala ya jinsia na wanawake mkoani Kilimanjaro,
(KWIECO) Clement Kwayu akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa shirika
hilo.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na maswala
ya jinsia na wanawake mkoani Kilimanjaro, (KWIECO) Elizabeth Minde
akizungumza wakati wa mkutano huo.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa KWIECO.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi
JUMLA ya wateja 1,660, wamepatiwa ushauri nasaha wa kisheriauliotolewa
na shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na maswala yajinsia
na wanawake mkoani Kilimanjaro, (KWIECO), katika mwaka 2012.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Bi Elizabeth
Minde, wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika makao mapya
ya shirika hilo yaliyopo eneo la Shanty town mjini Moshi.
Amesema katika kipindi hicho kambi nne za msaada wa kisheria ziliwekwa
na ushauri wa kisheria ulitolewa na kuwashirikisha jumla ya watu 1,020
huku kesi muhimu 62 kati ya 50 zilizopendekezwa zikifunguliwa
mahakamani katika kuongeza upatikanaji wa haki za wanawake na watoto.
“Katika kuongeza uelewa na ushiriki wa jamii katika kulinda haki za
Binadamu na jinsia, kamati za haki za Binadamu ziliundwa katika ngazi
za vijiji katika kata saba za Mkoa wa Kilimanjaro, ambapo mafunzo ya
uongozi yalitolewa kwa viongozi wa serikali za mitaa wapatao 318 hivyo
kuwajengea ujasiri katika kushughulikia masuala ya kijinsia na haki za
watoto”, alisema. Minde
Aidha Minde aliendelea kusema kuwa katika kuongeza uelewa, kulinda na
kutetea haki za watoto, mafunzo ya haki za watoto yalitolewa kwa
wajumbe 65, wanafunzi 960 na walimu 150, ambapo kamati saba za haki za
watoto na klabu 42 za watoto ziliundwa mashuleni.
Aliendelea kusema kuwa katika kuwajengea uwezo wa kiuchumi, jumla ya
wanawake 63 walioko maeneo ya pembezoni, walipewa misaada ya kujiajiri
wenyewe na 43 walipewa misaada kwenye ajira zisizo rasmi.
Minde alisema katika kipindi hicho cha mwaka jana, kiwango cha
umasikini miongoni mwa walengwa wa shirika hilo kilikuwa bado ni
changamoto kubwa, sambamba na ile ya watoto kutokuwa na uwezo wa
kuchangia mawazo yao mbele ya wazazi jambo ambalo alisema husababishwa
na tamaduni na imani potofu za kimila.
Shirika la wanawake, mwenyekiti mwanaume? iko kazi
ReplyDelete