Na A bdulaziz Video Lindi
Wakazi wa Manispaa ya Lindi, kwa takribani juma moja sasa,
wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa upatikanaji maji safi na salama na
kulazimika kutumia maji ya visima vya kienyeji vilivyochimbwa kwenye
baadhi ya makazi ya watu.
Baadhi ya wananchi waliohojiwa na Mtandao huu kuhusiana na tatizo
hilo, wameonesha hofu yao ya kutokea kwa milipuko ya magonjwa ya
matumbo ikiwemo kipindupindu kwa vile maji ya visima wanayotumia kwa
sasa siyo safi na salama kwa matumizi ya binadamu.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Maji safi na Usafi wa Mazingira
Lindi mjini(LUWASA), Idrisa Sengulo, pamoja na kukiri kuwepo kwa
tatizo hilo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Mamlaka,
amewaomba radhi wananchi kwa tatizo hilo ambalo amesema kama mambo
yakienda vizuri linaweza kutatuliwa ktk kipindi cha siku mbili zijazo.
Amesema mahitaji ya maji kwa wakazi wa Manispaa ya Lindi ni lita
milioni 5 kwa siku, ikilinganishwa na lita lita milioni 1,340,000 tu
kwa siku zinazopatikana kwa sasa.
Nadhani maji ni tatizo kubwa ambalo limefumbiwa macho na kubezwa na viongozi kwa kipindi cha tangu uhuru, juhudi za kuliondoa hili tatizo hazi akisi ukubwa wa tatizo licha ya utajiri wa vyanzo vya maji tulinao.Ifike wakati sasa tatizo la maji nalo lipewe kipaumbere kama malaria au kama tatizo la rushwa(japo ni propaganda).Maji ni uhai,maji ni afya, ebu jaribu kuangalia kiasi cha upatikanaji wa maji na matumizi yake kwa siku ktk taarifa hii ya huko lindi ndipo utakapo ona kwamba wengine wanakunywa tope au hata maji ya bahari ila hawasikiki kabisa.
ReplyDelete