Brother Michuzi,
Pole na kazi, asante tena na tena kwa kuendelea kutuunganisha sisi tulio ughaibuni. Najua nimesema hili mara nyingi, lakini lazima nirudie kusema kwamba kwa sisi tulioko nje wewe ndo chanzo kikubwa cha habari za nyumbani.. Leo naomba kuuliza wadau wa mtandao.. maelezo ya juu naomba weka kapuni.
Mimi ni mpenzi sana wa burudani ya matarumbeta(trumpets); nikiwa nyumbani hasa kwenye harusi bila tarumbeta naona mambo hayajaenda. Ila bahati mbaya nilivyoondoka Tanzania imekuwa vigumu sana kuzipata. Rais Obama alivyotembelea Tanzania akapigiwa matarumbeta huyoo kaanza kucheza, sasa nimesearch wee kwenye mtandao(hasa youtube) wapi, imagine mpaka naangalia harusi za watu nisiowajua ili kuona kama watapiga tarumbeta ila wapi.
Sasa nauliza wadau naweza kupata wapi CD, DVD au mtandao ambao una nyimbo za matarumbeta ya nyumbani? Nitashukuru sana msaada wenu
asante sana kaka
Nunua huko ulipo puliza tu utapata burudani
ReplyDeletePole sana wasiliana na wahusika wa Chuo cha maafisa wa magereza ukonga ama JKT mgulani utapata hayo , chuo ukonga magereza box 4283
ReplyDelete