Na Dixon Busagaga,wa Globu ya Jamii Moshi. 
 TIMU ya taifa ya Tanzania Taifa stars imerejea leo jioni nchini ikitokea Uganda ambako ilikuwa na mchezo wa marejeano wa kufuzu kucheza fainali za wachezaji wanaochjeza ligi za ndani (CHAN) 
 Kikosi hicho kimerejea majira ya saa 10:00 Jumapili jioni na ndege ya Precision na kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro ambako walipokelewa na viongozi mbalimbali wa chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro. 
 Msafara wa timu hiyo uliondoka uwanjanai hapo na kuelekea katika hotel ya Nyumbani iliyopo mjini Moshi ambako kulikuwa kumeandaliwa chakula na mapumziko kabla ya kwenda kupanda ndege kurejea jijini Dar es salaam. 
 Hata hivyo licha ya kipigo cha bao 3 kwa 1 kutoka kwa timu ya Uganda mashabiki wa soka katika mji wa Moshi walijitokea katika hotel hiyo kusalimiana na wachezaji huku baadhi wakionesha kusikitishwa na matokeo hayo.
 Wachezaji wa Stars wakiwa wamepumzika nje ya hotel ya Nyumbani mjini Moshi.
 Wachezaji wa Stars.
 Meneja wa timu ya Taifa Leopord Tasso Mukebezi akitambulisha mashabiki wa Stars kwa wachezaji wa timu hiyo.

Wachezaji wa Stars wakiingia kwenye gari tayari kuelekea uwanja wa ndege KIA kurejea jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2013

    sasa mmimi nahisi team ya Taifa stars ivunjwe kabisaaaaaa, halafu ziwekwe sura mpya, hawa washazoea kufungwa kwa hio sidhani tena kama watakuja fanya mabadiliko.

    hebu wahusika wekeni sura mpya kabisa kuanzia golikipa hadi watu wa ufundi.

    maana hakuna jipya tena taifa stars.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2013

    Kufungwa twafungwa ila chenga twawala.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2013

    hii timu ni ya wazembe tuu..wana wadhamini chungu nzima na pesa nzuri wanapewa lakini matokeo ni zero...ivunjwe tu waje wachezaji wapya...hawa hamna kitu nw!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 29, 2013

    cha kwanza hapo sie Tanzania tutaendelea kupoteza pesa nyingi kwa ajili ya kuwalipa makocha wa kigeni wakati wachezaji tulionao walishazeeka yaani mishe mishe za kukimbizana kiwanjani hawawezi misuli imezeeka,sana halafu wanakula vibaya wanakula viuzri tu wakiwa kambini sasa hapo timu hamna ,siku timu ikitengenezwa ndio vizuri ndio kocha wa kigeni atafutwe la sivyo tutakuwa tunapoteza hela.kuwa na kocha mzungu sio kuwa na timu nzuri tuangalie tunapokosea kwanza baadae ndio hawa watu watafutwe kwa jili ya kupanga wachezaji ambao walishaandaliwana sisi,sio kuwa na kocha mzungu basi tunaweka miguu juu ,itakuwa inakula kwetu kila mwaka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...