Bagamoyo 2
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid na Balozi wa Italia nchini Pierluigi Velardi wakizindua maabara ya kisasa kwenye majengo ya Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) huko Bagamoyo hivi karibuni. Maabara hiyo ambayo ina uwezo wa kutambua magonjwa mapya na yale ya hatari sana ikiwemo Ebola bila kuhatarisha maisha ya watafiti inajulikana kitaalamu kama Biosafety Lab 3, na ni ya kwanza ya aina yake katika eneo la Afrika Mashariki na Kati. Maabara hiyo yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.2 imejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Italia na inasimamiwa na Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI).
Bagamoyo 1
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr Seif Rashid hivi karibuni amezindua maabara ya kisasa kabisa ambayo ina uwezo wa kutambua magonjwa mapya na yale ya hatari sana ikiwemo Ebola bila kuhatarisha maisha ya watafiti inayojulikana kitaalamu kama Biosafety Lab 3 ambayo ni ya kwanza ya aina yake katika eneo la Afrika Mashariki na Kati. Maabara hiyo yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.2 imejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Italia na inasimamiwa na Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) kwenye maabara zake za Bagamoyo. Pichani anaonekana Mratibu wa mradi wa maabara hiyo Bw.Francesco Vairo akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afyya (wa pili kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dr. Rufaro Chatora na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi wakiwa ndani ya maabara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 31, 2013

    Ebola ni ugonjwa wenye asili yake Congo sioni sababu mitambo ifungwe Bagamoyo badala ya Kigoma. Misallocation of resources hiyo.

    ReplyDelete
  2. Msemaji wa kwanza naomba nikuelimishe kidogo. Hakuna asili ya ugonjwa wowote. Magonjwa hufuata binadamu kokote aliko. Uaweza kutoka nao Kigoma kwenda bagamoyo. Kigoma ukaisha ukajichimbia Bagamoyo n.k n.k

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...