Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akihoji bei ya maboga katika soko la Mombasa, wakati wa ziara yake ya kutembelea soko hilo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiangalia mboga mboga katika soko la Mombasa, wakati wa ziara yake ya kutembelea soko hilo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akihoji bei ya samaki katika soko la Mombasa, wakati wa ziara yake ya kutembelea soko hilo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akihoji bei ya nazi katika soko la Mwanakwerekwe, wakati wa ziara yake ya kutembelea soko hilo. Nazi moja inauzwa kati ya shilingi 200 hadi 400 (bei ya jumla).
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akihoji bei ya muhogo katika soko la Mombasa, wakati wa ziara yake ya kutembelea soko hilo. Fungu la muhogo linapatikana kwa bei ya shilingi 1000 hadi 2000.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akihoji bei ya muhogo katika soko la Mwanakwerekwe, wakati wa ziara yake ya kutembelea soko hilo. Fungu la muhogo linapatikana kwa bei ya shilingi 1000 hadi 2000.
huyu ndio kiongozi sio mambo yakukaa ofisini kuletewa habari kwamdomo.
ReplyDeleteAnon wa kwanza:
ReplyDeleteKama kweli twpima uongozi kwa vigezo hivi BASI tujitayarishe kwa majanga. Yeye alitakiwa aagize mtu afanye hilo na kumplekea taarifa siyo kuzurura na kufanya non-issues. Hii ni kutafuta cheap popurality. Kuna mengi ambayo angefanya badala ya kupoteza muda ktk masuala trivial kama haya
huenda meenda kununua futari,mbona asiende siku zote
ReplyDeleteHongera kiongozi
ReplyDeleteLakini nasikia kuwa bei ya mbatata, mihogo na kadhalika mwaka huu imekuwa balaa tupu.Watu hawawezi kupika traditional futari kwa bei za juu za vifaa.
Wewe Mdau wa Pili (2)hapo juu kwa Taarifa yako Uongozi ndivyo unavyoakiwa siyo kutuma Wawakilishi ama kupokea taarifa kwa njia za Simu.
ReplyDeleteUpo Dunia gani?,
Hukusikia siku zile kule nchini Chile Wachimbaji wa Madini walipofunikwa na kifusi kwa Miezi Mitatu (3) wakiwa chini aridhini , dunia iliona Raisi wao akishinda kwenye Kambi na Waokoaji hadi wote wachimbaji 33 wakaokolewa baada ya miezi mitatu arihdini...sasa unafikiri Raisi wa Chile angekaa Ofisini morali na ari ya waokoaji ingekuwepo?
Hujawahi kusikia mambo yakiwaharibikia Viongozi kwa kuendesha mambo kawa mtindo wa kupokea taarifa kwa njia ya simu?
Hujawahi kusikia Viongozi wakituma Wawakilishi na matokeo yake wawakilishi wakaboronga huku wakileta Ofisini taarifa za Upotoshaji na uongo?
Muda tulionao sio wa kuamini sana watu kwenye mambo yetu likiwemo la utendaji ktk uongozi.
Huyo ndio kiongozi anayejali anaowaongoza, angelikaa tu ofisini akapepewa na viyoyozi ila amaeamua kuona kwa macho siyo kupewa taarifa. Hongera na nimefurahishwa na kuona mifuko ya karasi tu hapo inauzwa na sio plastiki, tutunzeni mazingira yetu.
ReplyDelete