Picha na habari naa Dixon Busagaga 
wa Globu ya Jamii,Moshi 
 MTU mmoja ambaye jina lake halijafahamika mara moja amefariki Dunia huku wengine sita wakijeruhiwa vibaya kufuatia ajali mbaya iliyotokea juzi usiku majira ya saa moja katika eneo la Kawawa wilayani Moshi. 
 Majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa katika hosptali ya rufaa ya KCMC muda mchache baada ya kutokea kwa ajali hiyo iliyohusisha magari mawili likiwemo basi la abiria lijulikanalo kwa jina la Metro ambayo yaligongana uso kwa uso na Loli aina ya Fuso lililokuwa likielekea Dar es salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo  ilitokea baada ya dereva wa gari aina ya Fuso kujaribu kulipita Loli jingine aina ya Scania likiwa na trela lake kabla ya kukutana na basi la Metro lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Arusha ndipo magari hayo yakagongana uso kwa uso. 
 Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz alithibitsha kutokea kwa ajali hiyo huku akitaja namba za usajili wa magari yalihusika katika ajali hiyo kuwa ni basi la Metro aina ya Yutong lenye namba za usajili T 129 BQL likiendeshwa na Oscar na Fuso lenye namba za usajili T 615 AWB lililokuwa likiendeshwa na Goodluck Aseri.(45)lilikuwa likitokea Moshi kuelekea Njia panda Himo. 
 Kamanda Boaz alisema Dereva wa basi aliyefahamika kwa jina moja la Oscar alifariki dunia papo hapo huku kondakta na abiria wengie watano katika basi hilo walipata matibabu katika hosptali ya rufaa ya KCMC. 
 Alisema jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia Dereva wa Fuso kwa maelezo zaidi na kwamba mara uchunguzi utakapokuwa umekamilika atafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria za usalama Barabarani.
 Muonekano wa mbele wa gari aina ya Fuso baada ya kugongana uso kwa uso na basi a Metro baada ya kile kilichosemekana kuwa ni kupata hitilafu katika mfumo wa breki.
 Gari aina ya Fuso ikipakia mizigo iliyokuwa katika gari lililopata ajali baada ya kugongana uso kwa uso na basi la Metro na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
 Sehemu ya mabaki ya gari aina ya Fuso.
Dereva wa Fuso aliyefahamika kwa jina la Goodluck Aseri akiwa amelazwa katika hospitali ya KCMC akiwa na pingu mkononi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2013

    Kila barabara zikijengwa katika kiwango cha lami ndiyo ajali zinazidi kuongezeka.

    Inaonyesha dhahiri kwamba tumezoea 'vya kunyonga' vile 'vya kuchinja' hatuviwezi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 15, 2013

    Hii ndio vita yetu watanzania,tunakwisha tu, ukipiga mahesabu ya waliopotezana wanaopoteza maisha kwa ajali za barabarani yawezekana ukapata idadi sawa na idadi ya wanaofariki ktk civil war.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 15, 2013

    That is really humiliation, you get an accident and they tie you to a bed. Is that really a hospital? Should be sent to India or SA where the ruling class go, am serious!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 15, 2013

    vibaya sana wanavyofanya . Mtu amepata ajali si kwa uzembe ila ni matatizo kwenye mfumo wa break.

    Hapa najiuliza hawa wafunga pingu wana akili kweli?

    Lakini siwalaumu sana kwa sabb mswahili akinyanyuka hapo , nduki wala hasubiri kutoa maelezo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 15, 2013

    bongo tambarare! sirudi ng'o!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...