Taswira mbalimbali zinazoonesha maandalizi ya mapokezi makubwa ya Rais wa Marekani Barack Obama atapowasili Ikulu jijini Dar es salaam mchana huu. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama ilivyo kawaida yake amepita kila mahali kuangalia kwamba mambo yanaenda mswano, ikiwa ni pamoja na kusaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki.
Bendera zikiwa zimepangwa na kupangika katika upande wa lango kuu la Mashariki,Ikulu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia Kibao cha Barabara wa Barack Obama.






Kazi safi sana
ReplyDeleteDuuu!! Tanzania tunampokea Rais Obama kwa mbwembwe na upendo mwingi sanaa hakika!!! Lazima America itoe misaada mingi tu kweetu. Hakika hata Obama atafurahi sana namapokezi haya ya hali ya juu!!!!
ReplyDelete
ReplyDeletehahahaha hivi jamani watanzania kazi tufanya saa ngapi????? kwa mtondo huu umasikini hautoweza kuisha
duu eti Obama drive hahahhaa
hivi hawa watu wa kushangilia huwaga hawana shughuli za kufanya ama?Wanalipwa kwa kuwepo eneo la tukio
ReplyDeleteJamani ni heshima kubwa tumepewa ujio WA Obama NA si vibaya watu kujitokeza kwa wingi kumpokea. Kazi zitaendelea kama kawaida akiondoka.
ReplyDeleteHakuna kazi ya kufanya, watu wanapewa tshirts, kanga na vitenge na wanashinda siku nzima wakingojea Mmarekani. He is black but he is an american who is there for american interests. Wantanzania sisi watu wa ajabu sana, I would like to know how much it had cost to stage this unneceaary visit. Hizo hela zingweza kujenga shule kila kata nchini.
ReplyDeleteOOOh ni neema! haya tutaona
ReplyDeletePresident Obama tunakupenda na tunakujali na pia ni heshima kuichagua Tanzania katika ziara yako. Lakini ungetukubali na umaskini wetu, ungeijulisha serikali ya Tanzania wasitumie gharama zote hizo kwani kila shilingi moja tunaihitaji kwa maendeleo. Karibu Tena Rais Obama karibu tena Rais wa Marekani.
ReplyDelete