Mshauri Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer,Wine & Spirits Tanzania,James Rugemarila (kulia) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Wajibu wa Kutii amri ya Mahakama ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,baada ya kutokea uuzwazi wa Bia za Windhoek kinyume na taratibu kwa katika Hoteli ya Land Mark wakati bado Mahakama inaendelea kufanya kazi yake.hali hiyo imekuja baada ya kubainika kuwa unauza Bia za Windhoek ambazo ni za magengo.Kampuni ya Mabibo Beer,Wine & Spirits Tanzania ndio imepewa kibali na uhalali wa usambazaji wa Bia za Windhoek hapa nchini,zinazotengenezwa na Kampuni ya Namibia Breweries.Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mabibo Beer,Wine & Spirits Tanzania,Neil Stainton akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wakitoa taarifa ya uhalali wa usambazaji wa Bia za Windhoek zinazotengenezwa na Kampuni ya Namibia Breweries,leo kwenye Ukumbi wa Elkad 24,Mikocheni jijini Dar.
Meneja Mkuu wa Mabibo Beer,Wine & Spirits Tanzania,Neil Stainton akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wakitoa taarifa ya uhalali wa usambazaji wa Bia za Windhoek zinazotengenezwa na Kampuni ya Namibia Breweries,leo kwenye Ukumbi wa East 24,Mikocheni jijini Dar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mabibo Beer,Wine & Spirits Tanzania,Benedictor Rugemarila (kulia) akisisitiza jambo.





Inakkuwaje hii kampuni ipewe umiliki wa usambaji peke yake???soko huru la biashara liko wapi???mie sikubaliani nao hawa jamaa..biashara ni ushindani sio waachiwe wao tu hii ni karne 21!!
ReplyDeleteWewe ni hujui unaloongelea, wao ndio wanakibali kama sole suppliers nchini Tanzania hii kitu ipo duniani.
DeleteWao ndio wamekuwa wa kwanza kuleta bia hizo, sasa wanauza kwa bei ya kiwandani then ndio watu wananunua na kuuza kwa wateja.
Kuwa sole supplier basi hiyo hoteli ingeanza wao kupata bia hizo kabla ya hawa kuzileta na kuzitangaza nchini. Do you get that?
So wanaibia kwenda kuleta bia toka nje ya nchi bila kupitia kwa sole supplier.
Hapa niameandika ili ujifunze kama let's say kesho unapewa tender ya kufanya kitu hata tokea hapo bongo, unaambiwa ni wewe tu ndio utasambaza. Wateja wanaambiwa ni wewe etc
Kesho yake unakuta mtu mwingine anafanya kama wewe kweli utanyamaza? Na hapo umesha invest pesa kibao zako unasubiri faida irudi?
Acheni wivu wa kudandia kazi za watu na kusubiria mwishoni kuiba nyie haya mahakama itasema.
Inafurahisa kuona mke na mme wakishirikiana ki biashara. Si kawaida.Familia zingine, mke hajui mme ana nini na mme hajui mke ana nini. Mwisho wa siku mme akiondoka duniani anaondoka ki vyake na mke kadhalika. Nawashauri wenye maisha ya namna hii wabadirike vinginevyo wanadnaganyana
ReplyDeleteAnony wa pili msamehe huyo anony wa kwanza maana hajui dunia ya biashera inavyokwenda. Yeye akikopi rekodi ya mtu ya mziki anadhani ni sawa tu. Dunia ya biashara haiko hivyo. Mikataba lazima ihashimiwe. Ujanja ujanja haufai.
ReplyDelete